FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

FT: Simba 2-0 Yanga | NBC PL | Benjamin Mkapa Stadium | 16.04.2023

Kama ni uchawi basi ni wa moto, kwamba Kanoute kila derby inamkuta mgonjwa, tena ugonjwa ambao ni tofauti na majeraha ya kimpira? Au huwa anakwepa hizi game?

Kwa uwepo wa Nyoni dimba la kati, sioni tukitoboa hii mechi. Hapa ni either kipigo au draw.
 
Leo kuna watu watajuta kumjua Baleke!! Hat trick ya King Kibaden Mputa leo inajirudia! Baleke hata kama haumpendi utalazimika kumfurahia!!
 
Tusubiri watu waanze kulaumu kikosi sio
 
Mwanamuziki nguli wa Bongofleva, Lady Jay Dee aliwahi kuimba kibao maarufu " Siku hazigandi " alikuwa sahihi. Lile pambano lililokuwa linasubiriwa kwa hamu hatimae ndio linapigwa leo, ama kweli siku hazigandi.

Ndio ni Kariakoo Derby, ni Simba Sc Vs Yanga Sc katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar Es Salaam saa 11:00 jioni.

Mnyama mkubwa mwituni, Simba Sc itakuwa inawaalika wapinzani wao wa jadi Yanga, huku ikijaribu kupunguza pengo la point baina ya timu hizo mbili.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 68 huku Simba ikiwa na alama 60 hivyo kufanya tofauti kuwa alama 8 huku zikisalia mechi 5 kabla ya msimu kuisha.

Simba itashuka dimbani kujaribu kutafuta ushindi wake wa kwanza tangu ilivyofanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019. Ni mechi saba sasa Simba hajamfunga Yanga katika Ligi Kuu ya NBC.

Mechi ya mwisho walipokutana wababe hao, matokeo yalikuwa 1-1 kwa magoli ya Augustine Okrah kwa Simba na Aziz Ki kwa upande wa Yanga.

Simba itashuka dimbani huku ikimtegemea zaidi mshambuliaji wake aliyefomu , Jean Baleke ambaye kwasasa hakamatiki kwa fomu yake huku akina Chama, Ntibazonkiza na Mzamiru wakitegemewa kuleta chachu ya ushindi.

Kwa upande wa Yanga, watamtegemea zaidi Straika wao ambaye fomu yake imekuwa ikipanda na kushuka Fiston Kalala Mayele huku pia Aziz Ki na akina Jesus Moloko wakitegemewa kunogesha zaidi.

Je, Simba atakubali kuendelea kuwa mnyonge kwa Yanga?
Na vipi upande wa pili, ubingwa bila kumfunga mtani unaweza kunoga?

Mwamuzi wa mtanange huo ni mwanamama, Jonesia Rukya akisaidiwa na akina Janeth Balama pamoja na Mohamed Mkono.

Mechi ni saa 11:00 jioni na itakuwa live Azam Sports 1HD

Kwa live updates, utani wa hapa na pale na yote yanayohusu mechi hii basi hapa ndio sehemu sahihi kwako Mwana JF...

View attachment 2589925
Kikosi cha Simba
View attachment 2589930
Kikosi cha Yanga​
Wacha nitie signature iwe ni kumbukumbu kwa vizazi!
 
Hapana kaka WACHEZAJI wengi hawapo, mfano Beno yeye amesha Saini singida big stars Hapo amekuja tu kuongeza idadi ya makipa, kanoute majeruhi tukubali tu Simba kikosi kidogo
mudi anauza hadi vijiko kabatini tulie mikono

babra nae tulimwamini tukamtuma gengeni matokeo yake ananunu makachakacha kina okwa hawa watu wanatuchukuliaje
 
Kama ni uchawi basi ni wa moto, kwamba Kanoute kila derby inamkuta mgonjwa, tena ugonjwa ambao ni tofauti na majeraha ya kimpira? Au huwa anakwepa hizi game?

Kwa uwepo wa Nyoni dimba la kati, sioni tukitoboa hii mechi. Hapa ni either kipigo au draw.
Yaan kwa nyoni hapoo hadi kimuhe muhe kimekataa, wallah hakuna maajabu tena hapaa.
 
Back
Top Bottom