FT: Simba 2 Geita Gold 1 NBC Premier League

Swala la waamuzi katika soka imekuwa ni gumzo ulimwenguni kote

Ndo maana wazungu wakaja na VAR lakini bado watu wana nung'unika tu

Kwenye hili shabiki wa izi team pacha tuwe na akiba ya maneno
 
Kipindi geita wanafunga bao la pili refa alikuwa mbali lakini katika harakati za kugombea ule mpira mchezaji wa simba alianguka kabla ya mpira kuingia wavuni, ilikua physical contacts mixer na distance so mwamuzi akatafsiri kama nilivyopenda iwe
 
Basi tufanye hilo moja wamebebwa Simba tusilihesabu lakini si bado walikuwa wanaongoza 2? Tofauti na utopwenga wasingebebwa kule Lindi dhidi ya Namungo tungekuwa tunaongea nini leo?
Kama Simba na Yanga zisingebebwa maana yake mpaka raund hii Simba angekuwa amepoteza point 6 na Yanga angekuwa amepoteza point 3 tu.
 
Ni kwamba Geita Gold wamefunga, goli likakataliwa

Ilikua hivi, mchezaji wa Geita aliyefunga alikua nyuma ya Kapombe, Kapombe aliruka akaukosa mpira, ikabidi ajiangushe, Refa akatafsri amesukumwa ilihali hakusukumwa alijirusha tu mwenyewe na ubwege wake

Na mfungaji wala hakutumia nguvu kuruka, yaani ni aibu kukataa lile goli, ila ndio hivo tena!!!
 
Sijakataa ila kwa mustakabali mzuri wa afya yangu, acha iwe hivyo tu
Hii mechi ni kama SI unit ya kupima uzalendo wa wanayanga uko wapi. Kipimdi nyinyi mnabebwa ili msawazishe baada ya kufungwa hakuna aliyeweza kupinga maamuzi ya refa kwa wakati ule kwasababu timu yake ilikua katika point ngumu ya kupoteza mchezo

Tulisema sana siku ile kwamba haikua fair lakini wote mlibaki kufurahia matokeo na kuacha kabisa kujadili mazingira ya penalty yalivyo patikana
 
Hii ni aibu kwa soka letu. Kwa issue ya yanga na Namungo unaweza singiziaa kua Feisal alichezewa faulo na ukaning'inia hapo. Hii ya kapombe watu wataning'inia wapi?

Mpira wa tz ni aibu sana. Aibu kubwa sana.
 
Kwa kweli mashabiki wengi wa simba ni tofauti na wa upande wa pili. Hapa mashabiki wengi wa simba tunakiri kubebwa na timu kucheza vibaya. Wa upande wa pili wao lawama huwa ni kwa tff na waamuzi hata timu yao ikiwa mbovu.
 
Kipindi geita wanafunga bao la pili refa alikuwa mbali lakini katika harakati za kugombea ule mpira mchezaji wa simba alianguka kabla ya mpira kuingia wavuni, ilikua physical contacts mixer na distance so mwamuzi akatafsiri kama nilivyopenda iwe
Mnazi wa makolo Leo ,mbebwa live bila chenga , ww msimu huu utapata presha wallah hahahaha maana c kwa unazi huu
 
Hii ni aibu kwa soka letu. Kwa issue ya yanga na Namungo unaweza singiziaa kua Feisal alichezewa faulo na ukaning'inia hapo. Hii ya kapombe watu wataning'inia wapi?

Mpira wa tz ni aibu sana. Aibu kubwa sana.
Naona una halalisha mbeleko yako dhidi ya namungo kwa kutumia faulo ili ionekane halali

Mbona hata mazingira ya goli la leo unaweza uka apply sheria hiyo hiyo kwa kusema mchezaji aliyeanguka kabla ya goli kuingia alifanyiwa faulo na ika-make sense tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…