FT: Simba SC 1-0 Jamhuri SC | Mapinduzi Cup | New Amaan Complex| Robo Fainali | 08.01.2024

FT: Simba SC 1-0 Jamhuri SC | Mapinduzi Cup | New Amaan Complex| Robo Fainali | 08.01.2024

Asante sana Modes.
Leo mmekuja mapema sanaaa.
 
Match Day

Simba SC Vs Jamhuri SC
Mapinduzi Cup
New Amaan Complex
Robo Fainali
08.01.2024
View attachment 2865422
Mchuano huu ni kwa ajili ya mchezo wa soka uliosubiriwa kwa hamu huku robo fainali ya nne ikiendelea leo saa 2:15 Usiku kwa kuwakutanisha Simba SC dhidi ya Jamhuri FC katika Uwanja wa Amaan.

Mchezo muhimu huu unaweza kuamua ni timu ipi itakayopata nafasi ya kutia mguu wake kwenye nusu fainali ya mashindano haya.

Huku baadhi ya timu kama APR na Mlandege tayari zikiwa zimefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali, shauku kati ya mashabiki wa soka Tanzania iko juu

Mashabiki kote kwenye visiwa na Tanzania kwa Ujumla wanasubiria kwa hamu matokeo ya mchezo kati ya Simba SC na Jamhuri FC ili kujua ni timu ipi itakayosonga mbele kuingia nusu fainali. Kukutana na Azam FC au Singida FG ambao mechi yao itapigwa mchana wa leo.(nitakujuza matokeo yao pia)

Uwanja wa Amaan umekuwa uwanja wa vita kwa mchezo huu mkali, ambapo ujuzi, mkakati, na azma vitacheza jukumu muhimu katika kuamua mshindi.

Mimi Uran, nitakuwa tayari kukupa updates za mchezo huu kwa ueledi na kwa upana kabisa .

UPDATES ....

Mechi ya Azam vs Singida FG
imemalizika kwa Azam kukubali kichapo cha Goli 2-1.
View attachment 2865600

Singida FG anasubiria Mshindi Kati ya Simba na Jamhuri kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali utakaochezwa Kesho kutwa.

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA
View attachment 2865633


Tukutane Baadae .....

All the Best Mnyama.
#nguvumoja#
Utabiri,

Simba3,
Jamhuri 1
 
Simba wako serious kuliko userious wenyewe 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Watachezea za kutosha kabisa
 
Che Malone huwa ana ugonjwa wa kulazimisha kupiga pasi za mbele katikati ya msitu wa wachezaji pinzani, hili nimeliona mara nyingi sana na mara zote huambulia kupoteza mpira.
 
Back
Top Bottom