Mnyama Mkubwa Mwituni asiyefugika, Simba Sports Club anashuka dimbani leo kuikabili Horoya AC katika mchezo muhimu wa kundi C.
Simba itaingia uwanjani ikiwa na alama 6 huku Horoya wakiwa na alama 4. Ushindi wa aina yoyote utawafanya Simba wafuzu robo fainali.
Leo ni ama afe kipa au afe beki, ushindi ni lazima kwa Mnyama, na kwa uzoefu wangu, mechi za namna hii Simba akiwa kwa Lupaso huwa tunashinda goli zisizopungua 3.
Shime wana Simba tujitokeze kwa wingi hapo Lupaso ili tukahanikize ushindi wetu mapema, najua friends of Horoya watakuwepo ila hawatosumbua.
Mchezo utakuwa mubashara saa 1:00 usiku na kama kawaida, ZBC 2 ya AzamTv na Variety 4 ya DStv watakuwa live.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba Sports Club. 🦁🦁🦁