FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

FT: Simba SC 7-0 Horoya AC | CAF Champions League | Benjamin Mkapa | 18.03.2023

Dah yaani huwa hamtaki kabisa kukubali uwezo wa mnyama! Lazima mtafute sababu tu ya kumdharau. Hivi simba angefungwa leo ungeandika ulivyoandika? Mkuu mpira ni wa uwazi kabisa ifike wakati tukubali uwezo wa simba, kwa leo simba wamebadilika sana tofauti na mechi tatu zilizopita. Makosa waliyoyafanya horoya ni ni kuidharau simba wakiamini wanaweza kufanya chochote matokeo yake wakakutana na simba iliyoimarika sana leo wakapotea mazima kilichofuata ni 7 bila.
ana uwezo gani
si huyu alikandwa 3 kwake
si huyu alikuwa anashinda goli moja, moja kwa kibonde vipers sasa ana uwezo gani
sema mgomo wa horoya ndio umembeba ila kwa uwezo wote mnajua hana lolote
 
umesoma ukaelewa
hii taarifa ni ya mzunguko wa kwanza na walimkanda simba wakachukua dola 5000

mzunguko wa 2 wakaambiwa wakipaga goli ni m100 wakapata, raisi akawageuka hakuwapa ndo mechi hii wamekuja kukamilisha tu

unanambia hawana shida ya pesa vipi, kwamba hizi bonus huwa hawachukui wakishinda
kwamba wao wanacheza kupata bonus tu?
 
hahahaha horoya alikuwa na mgomo, uliwahi ona ligi ya mabingwa kipa anadaka vile

unaoigwa 7 wana hujutii unafurahi
hujui mpira wewe, goli 1 ndio wachezaji wanajutia utaona wanalala uwanjani mana wanaona kama wangeweza kufanya Jambo, Ila goli 7 wanakua washakata tamaa kisaikolojia baada ya kufungwa 3, morali inashuka
 
hujui mpira wewe, goli 1 ndio wachezaji wanajutia utaona wanalala uwanjani mana wanaona kama wangeweza kufanya Jambo, Ila goli 7 wanakua washakata tamaa kisaikolojia baada ya kufungwa 3, morali inashuka
unajutia kama ulikuwa na uhitaji wa nafasi horoya anajuta vipi alikuja na wazo la kukamilisha ratiba tu

uliona man u baada ya kula 7, wakitoka na furaha na bashasha
 
Hongera Mtani

Finali hii hapa...Shida ni Mamelodi na Al Ahly. Mkitoboa hapo huyu hapa Raja Casablanca kwenye fainali
Al Ahly hatuwezi kukutana nae maana akifuzu atakuwa nafasi ya 2.
Timu za nafasi ya 2 zote haziwezi kukutana.
 
Fix sana we jamaa.. leo mtapigwa kipigo cha mbwa koko,kipigo ambacho chozi lake litawatokea ulimini! Kipigo Chenye pigo lisiloisha ukali wake!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

20230318_214841.jpg
 
unajutia kama ulikuwa na uhitaji wa nafasi horoya anajuta vipi alikuja na wazo la kukamilisha ratiba tu

uliona man u baada ya kula 7, wakitoka na furaha na bashasha
Hoja dhaifu mno... Hata Eng. Hersi & Luc Emayel wamewachoka.
 
Horoya kwa namna wanavyocheza ilikuwa halali wapigwe nyingi, kwanza awakumuheshimu mpinzani ambaye yuko nyumbani kwake, wameingia kwenye mchezo wakafunguka kuanzia dk ya kwanza ya mchezo, na hapo hapo wakashindwa kujielewa kwamba sio wazuri ni timu ya kawaida sana ambayo nafikiri bado wanajitafuta ili kurudi kwenye ule ubora waliokuwa nao misimu miwili iliyopita ambapo waliuza wachezaji wengi sana na kuacha wengi pia, Sasa unapokutana na timu kama hii basi zitumie nafasi unazopata kiuhakika na ndicho walichofanya simba leo, kujisifu sana pia dhidi ya timu kama hii napo sio sahihi sana, unaweza ukajiona bora kumbe uliyekutana nae pia ni garasa, Ongereni jiandaeni vizuri dhidi ya wanaokuja kwenu ambao sio tena horoya bali ni timu aswaaa
Kwamba Horoya ni garasa?, huu ni uongo wa mchana wa jua kali kabisa, Horoya mpaka anafika hapo unafikiri Kapaa? Si alizifunga team kadhaa huko nyuma, angekuwa mbovu au kiwango kimeshuka angeangukia kwa "loosers" hii ni Champions league hakuna team dhaifu hapo. Horoya ni moja ya team nzr sana kwa ukanda wao na wako na wamekuwa wakishiriki constantly haya mashindano. Juzi tu Alhy kala 5 na Mamelody, kwahy hawa si ajabu kula 7, ni kwamba ukiingia kwenye mfumo tu, umekwisha, jana Horoya kaingia cha kike.
 
walihaidiwa na hawaja pewa, mbaya zaidi wakageukwa
horoya wa kumkazia raja kwao aje apigwe 7 na huyu nyau wa kuunga unga hushangai
Daahh..kaka unahangaika na Simba yaani Toka Jana unasema Simba ameshinda kibahati Bahati ,punguza baasii wivu na chuki hata km huipendi Simba wamefanya vzr na hakuna goli la bahati mbaya
Man U walipigwa Saba na Liver utasema nao walikua na mgomo?
Simba wameshinda Kwa kua wamestahiki brooo...leave that chuki,pole Sana sijui km ulilala usiku wa kuamkia leo
 
Back
Top Bottom