FT: Tanzania 1-0 Niger | AFCON Qualifier | Estadio Benjamin Mkapa | 18.06.2023

Uganda ashapigwa mbili huko... habari nzuri kwa Taifa Stars
 
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeicharaza timu ya Niger goli 1-0 na kufufua matumaini ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2023 nchini Ivory Coast.

Saimon Msuva mfungaji wa goli hilo ndiye shujaa wa mchezo huo uliochezwa Juni 18, 2023 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amewaongoza watanzania kuishangilia timu yao akiwa Mgeni Rasmi katika mchezo huo hatua iliyoongeza hamasa.

Mchezo huo umeshuhudiwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Naibu Katibu Mkuu wake Bw. Nicholas Mkapa, Rais wa Shirikisho la Mpira nchini (TFF) Wales Karia.

Tanzania ipo kundi F pamoja na timu za mataifa ya Algeria, Niger na Uganda kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).View attachment 2661798View attachment 2661800View attachment 2661801View attachment 2661802View attachment 2661804View attachment 2661803View attachment 2661805View attachment 2661806
 
Tanzania haina kiwango cha kucheza Afcon.
Bora waingie Uganda.
 
Club zina option ya kusajili wachezaji tokea nje. Tatizo kubwa tulionalo ni wachezaji wetu kuwa watu wa kuridhika na vitu vidogo hawana ambition ya kufika mbali kisoka

Afcon ni platform kubwa ya kutangaza vipaji vyao ilipaswa wawe wanajituma sana ili wapate fursa ya kwenda afcon ili wapate timu kwenye mataifa yaliyopiga hatua kisoka

Sema ndio ivo wameridhika na kuchezea nyumbani
 


kama unajua mpira, utajua kuwa swala sio kusajili tu wachezaji nje, bench la ufundi lina mata sana.

Unai Emery, kocha Mspain aliichukua Aston Villa ikiwa na wachezaji wale wale ambao makocha wengine walishindwa kufanya nao vizuri na kuipeleka UEFA.

Ndio maana Alexander The Great alisema, "I am not afraid of an army of lions led by a sheep; I am afraid of an army of sheep led by a lion. Alexander the Great"

Akimaanisha "Siogopi jeshi la Simba linaloongozwa na Kondoo; Ninaogopa jeshi la Kondoo linaloongozwa na Simba"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…