FT: Tanzania Prisons SC 1-3 Simba SC | NBC Premier League | Sokoine Stadium | October 5, 2023

FT: Tanzania Prisons SC 1-3 Simba SC | NBC Premier League | Sokoine Stadium | October 5, 2023

JamiiForums1979314066.jpg

Msimamo
 
Leo onana kwa dk chache alizocheza kaonesha anahitaji kuanza, phiri anahitajika kikosi cha kwanza.

Saidoo kwanini kataka kupiga yeye ile penati, ni ubinafsi, kwa kipindi kigumu anachopitia phiri anahitaji support toka kwa wenzie.

Simba viongozi walisajili hovyo, kuna watu wanahitaji kupewa nafasi ili waweze kujianini wafanye vitu vyao kwa uhuru, mfano chama akikosea hana tabu sababu wala mashabiki hawatalalama sana sababu alishaonesha uwezo wake.
Ila onana akikosea atakuwa na mashaka, na kitu hicho ndio kinawatoa wachezaji mchezoni.

Chilunda anahitaji muda zaidi.. msimu huu uwe wa mwisho kwa boko, kazi na umri.

Kibu akiongeza matumizi ya akili badi ni mchezaji mzuri saana.

Saidoo bado anacheza mpira wa gombania goli(mpira wangu) ule ni mpira wa shule(anao anao)

Mzamiru anahitajika msaidizi wake mnyumbulifu zaidi.


Sina shida na ally salim, nina shida na waolalamikia salim awe kikosi cha kwanza, mie kwangu bado.
Saidoo hana goli ligi kuu, alitaka kuondoa gundu

Kibu nguvu nyingi akili kidogo

Kennedy ni bonge la beki
 
Ligi ya 5 Afrika ni ngumu kuamini kama JW kuwa wa 6 Kwa ubora duniani.
 
Naangalia hapa mpira wa Chama langu Simba na prison, ninayo yaona nafsi imekataa kabisa kuamini kwamba hii ni ligi ya tano kwa ubora kama tunavyoaminishwa, sasa napiga picha hiyo ligi ya mwisho kwa ubora sijui wanachezaje.
Hizo ligi zingine umeangalia?
 
Back
Top Bottom