FT: TZ Prisons FC 1-2 Yanga SC | NBC Premier League | Sokoine Stadium | 11.02.2024

FT: TZ Prisons FC 1-2 Yanga SC | NBC Premier League | Sokoine Stadium | 11.02.2024

Wakati mwingine muwe fair. Refa amejitahidi sana kuchezesha vizuri kwenye huu mchezo.

Marudio yameonesha wazi yule mshambuliaji alikuwa anatafuta penati. Kwa hiyo alistahili kabisa kupewa kadi ya pili ya njano.
Amepewa kadi kwasababu aliushika ule mpira.
Na ni Nondo alimpiga push
 
Hii yanga ya sasahivi sio ile ya kabla ya disemba waliyompiga simba 5 , sasahivi wanacheza kichovu sana . Hawakabi watatu watatu Kama mwanzo , haikimbizi spidi Kama ya zamani , mwamnyeto anacheza Kama Mzee wa Miaka 70.
Dakika za mwisho wanashikilia bomba haikuwa style ya yanga hii .
Hawa wachezaji itakuwa wamezamishwa Kwenye mabwawa ya mademu wa Daressalaam.
Huu ushindi wa kufurahia sana sio style ya ushindi wa yanga hii .
Kwa kifupi mabaki ya falsafa ya Nabi yanaishilia. Hadi June tutakuwa na timu isiyo na mabaki ya Nabi
 
mmekoswa koswa sana
Uko sahihi. Prisons ya sasa siyo ile ya kubutua tu mpira na kutumia nguvu nyingi. Prisons ya sasa inacheza mpira mzuri malengo, na pia wa kuvutia.
 
Back
Top Bottom