FT: Yanga 1-1 Al Hilal Club (CAF Champion League) | Mkapa Stadium | 8-10-2022

FT: Yanga 1-1 Al Hilal Club (CAF Champion League) | Mkapa Stadium | 8-10-2022

Mechi nane zilizopita nne mnyama kakalia chuma,zote ni ngao!?..Simba ikicheza ngao na ikicheza caf mzamiru anakua tofauti!?
Huwezi kuelewa naona wewe labda umewahi kucheza rede tu. Wachezaji wanatumia energy tofauti kutokana na mpinzani alivyo vile vile kutokana na mashindano.

Hii energy mliotumia Leo haiwezi kuwa Sawa mngekutana na Al hilal mechi ya kirafiki dhidi ya wachezaji hao hao.
 
Leo uzi umeendaa ila nyie Simba sio wa njiii hii mmeujaza udhi wa watu nyeee.
 
FULL TIME
90' Zinaongezwa dakika 4
89' Wageni wanafanya shambulizi kali lakini Diarra anaokoa
80' Kasi ya mchezo inazidi kuongezeka, Yanga wanaendeleza kasi kutafuta goli la pili
75' Shuti la Mayele linagonga nguzo na kurejea uwanjani
73' Al Hilal wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona, ya tatu kwa AL Hilal
72' Yanga wanapata kona ya 11, anapiga Aziz Ki inaokolewa
70' Al Hilal wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka nje
Abdulrahman Yusuph anaisawazishia Al Hilal
67' GOOOOOOOOOOOOOOOO
64' Morrison anachezewa faulo
60' Mayele anakosa nafasi ya wazi baada ya mpira kuwa na kasi
54' Kasi ya mchezo imeongezeka kwa timu zote
Mayele anaipatia Yanga goli la kwanza kwa shuti la nje ya 18
52' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
46' Yanga wameanza kwa kasi
Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

45' Yanga wanapata kona, Ki anapiga inaokolewa
44' Al Hilal wanaruhusu lango lao kufikiwa mara kwa mara
40' Yanga wanarejesha kasi yao waliyoanza nayo lakini wapinzani wao wapo makini
31' Yanga wanapata kona, anapiga Aziz Ki shambulizi linaokolewa
28' Al Hilal wanapanga mashambulizi taratibu
25' Kasi ya mchezo imebalansi, timu zote zinamiliki mpira kwa zamu
20' Al Hilal wanapata faulo nje ya 18 ya eneo la Yanga
19' Wageni wametulia na sasa wanapiga pasi kadhaa, wamefika langoni mwa Yanga kwa krosi
12' Shambulizi kali langoni mwa Al Hilal Club lakini walinzi wanaokoa
11' Morrison anawatoka walinzi, mpira unambabatiza beki inakuwa kona nyingine
10' Yanga wanapata kona
4' Yanga wanafanya shambulizi la kushtukiza, inakuwa kona, inapigwa haizai matunda
3' Presha ya mchezo ipo juu lakini ni Yanga ndio wanaomiliki mpira muda mwingi
1' Yanga wanafanya shambulizi kupitia kwa Morrison, inakuwa kona

Mchezo umeanza, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo


View attachment 2380734
Kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa leo Oktoba 8, 2022

================
Wakuu leo ndiyo leo, mtoto hatumwi dukani, ngoma ya mtoto haikeshi, usiku wa deni haukawii kukucha.

Leo majira ya saa 10:00 jioni, katika dimba la Benjamin Mkapa, Yanga watashuka dimbani katika mchezo wao dhidi ya Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Ikumbukwe, katika michezo yao ya awali, Yanga waliwatoa Zalan na Al Hilal wakawatoa St. George ya Ethiopia.

Yanga inafundishwa na Kocha Prof. Nabi huku wapinzani wao wakinolewa na Kocha Ibenge. Iwe jua iwe mvua timu ya Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia goli 3 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.

Mechi itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 1HD.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile ajpp
Rudisha kwao hao wakongo,hawana msaada.
 
Aisee
 

Attachments

  • 0d82e68bf6b149d48aaddcf4762e8ff6.mp4
    1.2 MB
Dalili ya simba kufungwa na Agosto ni kushangalia sare ya yanga.


Mchezo wa leo ulitawaliwa na pressure wachezaji wanahitaji kuwa calm na pia Kocha nabi ajofunze kupambania kipindi cha kwanza hawa jamaa walipaswa kufungwa first half na kimaliza game second

Hatuwezi kwenda khartoum na kucheza kama tunategeana tunatakiwa kuwasha moto kweli kweli
Sijui ni uchawi!!!! Yani nlishangaa Yanga walivyochanganyikiwa. Hovyo kabisaa
 
Focus imeamia NBC baada ya kuona CAF pagumu?

Kwa malengo yenu hayo basi ile record yenu ya 1998 mtakuja kuivunja 2060
Kikubwa tunakupakata 'kila mtu na d.em.u wake'sauti ya mr nice
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Uzuri ni kwamba furaha kwa mashabiki bado ipo

Furaha ni kuona Yanga ikizidi kucheza mechi yake ya 44 bila kupoteza, naam hicho kwetu kina maana kubwa sana
Naam...
 
Back
Top Bottom