FT:Yanga 1 - 1 Malindi

FT:Yanga 1 - 1 Malindi

Kwani Yanga wanasemaje juu ya hilo
Shadeeya njoo mara moja hapa pia usisahau kuja na matikiti.
Nini lakini Mtani.

Yanga logo.jpg

SOMA HIYO MTANI.
 
Aisee naona umewasili sasa hayo matikiti yako wapi
Jamaa wameoga,wamefua na wamepasi na hivi sasa wako mjini, wanataka kumshikisha adabu Chura nyumbani kwake.
Je ni kina nani hao? Shadeeya
Mpira una matokeo Matatu lakini Mtani ikitokea hivyo pia sio mbaya.

Najua watapata mashabiki wengi tu ila tupo ngangari kuhakikisha tunapata matokeo nyumbani. Karibu Mtani.
 
Yanga walianza kufunga first half kupitia kwa Deus Kaseke, na baadaye kwenye dakika za lala salama (dk.94) Malindi wakasawazisha na hivyo mpira kuisha kwa magoli 1 - 1.

Niliyobaini kwenye mechi hii:

Kwanza;inaonyesha Yanga hawajajipanga kwa michuano mikubwa.Kwanini nasema hivyo?Huwezi kusema eti unaenda kushindana kwenye CAF CL huku kwenye maandalizi unacheza mpira wa hovyo,usio na mipango namna ile.

Pili;Kuna maeneo Yanga wamejitahidi kusajili.Nawapongeza kwa kuwa na Mohammed Issa 'Mo Banka', Deus Kaseke mpambanaji,na wengine wachache.Hawa jamaa wanajituma kwakweli,lakini wengine mmmmhhh...!!

Tatu;Huyu mchezaji mliyetufanyia surprise (David Moringa) ni mzigo kwa timu,yaani kwa huyu watani zetu mmepigwa mkapigika hasa.Hivi mlisajili mcheza soka, mbeba vitu vizito au bodyguard? Mechi dhidi ya Kariobangi nilimwona anaruka ruka tu kwenye zile dakika 5 alizopewa.Leo kafanya yale yale kwa dakika takribani 70.
Eti mlikuwa mnasema Simba imeibiwa kwa wale Wabrazil?Nyie itakuwa ni zaidi ya kuibiwa.

Anyway,watani zangu mna nafasi ya kujipanga kwa ajili ya TPL tu,huko kwingine wala msisumbuke.Na kwa aina ya wachezaji mlionao, malengo yenu mwaka huu nadhani ni kuishia nafasi ya 3 kwenye TPL.Mnasikitisha!😱
Mikia FC kazini.
 
Yanga walianza kufunga first half kupitia kwa Deus Kaseke, na baadaye kwenye dakika za lala salama (dk.94) Malindi wakasawazisha na hivyo mpira kuisha kwa magoli 1 - 1. Niliyobaini kwenye mechi hii: Kwanza;inaonyesha Yanga hawajajipanga kwa michuano mikubwa.Kwanini nasema hivyo?Huwezi kusema eti unaenda kushindana kwenye CAF CL huku kwenye maandalizi unacheza mpira wa hovyo,usio na mipango namna ile. Pili;Kuna maeneo Yanga wamejitahidi kusajili.Nawapongeza kwa kuwa na Mohammed Issa 'Mo Banka', Deus Kaseke mpambanaji,na wengine wachache.Hawa jamaa wanajituma kwakweli,lakini wengine mmmmhhh...!! Tatu;Huyu mchezaji mliyetufanyia surprise (David Moringa) ni mzigo kwa timu,yaani kwa huyu watani zetu mmepigwa mkapigika hasa.Hivi mlisajili mcheza soka, mbeba vitu vizito au bodyguard? Mechi dhidi ya Kariobangi nilimwona anaruka ruka tu kwenye zile dakika 5 alizopewa.Leo kafanya yale yale kwa dakika takribani 70. Eti mlikuwa mnasema Simba imeibiwa kwa wale Wabrazil?Nyie itakuwa ni zaidi ya kuibiwa. Anyway,watani zangu mna nafasi ya kujipanga kwa ajili ya TPL tu,huko kwingine wala msisumbuke.Na kwa aina ya wachezaji mlionao, malengo yenu mwaka huu nadhani ni kuishia nafasi ya 3 kwenye TPL.Mnasikitisha!😱
Nyinyi mnataka wacheze vipi ?
Je timu za Zanzibar ziliweka wapi kambi? ??
Mbona mna matatizo sana na Yanga?
 
Back
Top Bottom