FT: Yanga 2-0 Pamba Jiji | Ligi Kuu NBC | KMC Complex | Yanga wanagawa dozi tu

FT: Yanga 2-0 Pamba Jiji | Ligi Kuu NBC | KMC Complex | Yanga wanagawa dozi tu

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Yanga SC imeendelea kutoa dozi katika Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Max Mpia Nzengeli na Cheick Touré, huku Yanga ikiongeza pointi nyingine muhimu kwenye msimamo wa ligi.
================

Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans (Yanga), leo Ijumaa Agosti 28, 2026, wanatarajiwa kushuka dimbani kuikabili Pamba Jiji katika mchezo wa mzunguko wa nne wa ligi hiyo.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 3:00 usiku katika Uwanja wa KMC Complex, huku Yanga wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri baada ya kushinda michezo yao yote mitatu ya mwanzo msimu huu.

1787915684974.png


1787916299910.png
 
Mlezi w Pamba jiji ni mjumbe wa bodi na shabiki gala gala wa yanga,,.hakuna mechi hapo
 
Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans (Yanga), leo Ijumaa Agosti 28, 2026, wanatarajiwa kushuka dimbani kuikabili Pamba Jiji katika mchezo wa mzunguko wa nne wa ligi hiyo.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 3:00 usiku katika Uwanja wa KMC Complex, huku Yanga wakiingia kwenye mchezo huo wakiwa na rekodi nzuri baada ya kushinda michezo yao yote mitatu ya mwanzo msimu huu.

View attachment 3658834

View attachment 3658845
Yanga ni timu hatari na nusu
 
Hii yanga 🙌🙌

Baraza timu yake imepigwa goli 2 badala ahuzunike anasherekea kufungwa 2😄🙌
 
Mimi naona game plan ya mwalimu ilikuwa ni nzuri. Mnaolalamika mnatakiwa kujitafakari. Timu imeshinda 2-0! Ushindi ndiyo muhimu.
 
Back
Top Bottom