FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

FT: Yanga 2-1 Simba | Yanga yatwaa Ngao ya Jamii

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Timu zote zimeshaingia uwanjani.

Mchezo umeanza

01' Yanga wanamiliki mpira wakipiga pasi kadhaa.

11' Kibu Denis anaachia mkwaju na kuishia kwenye nyevu za pembeni

15' ⚽Gooooooal, Pape Sakho anaweka kimiani goli la kwanza la mchezo, krosi maridadi kutoka kwa Chama

19' 🟨Aucho anapewa kadi ya njano

22' Kona ya kwanza ya mchezo inachongwa na Yanga, almanusura Aziz Ki aweke uwanja sawa

23' Inonga anamjaribu Diarra kutoka nje ya 18 lakini anakuwa makini na kuupangua nje

24' Mohammed Hussein anachonga kona ya kwanza ya Simba, mpira unakosa manufaa

33' Feisal anaenda chini baada ya kukwatuana na Mkude, free kick ya Yanga inashindwa kuleta matokeo kwa kuleta offside

37' Simba wanapata freekick nje kidogo ya 18, Kanoute anajaribu kuunganisha krosi ya Chama lakini Diarra yuko makini.

42' Mlinda mlango wa Simba yuko chini akitibiwa maumivu ya misuli

45+1' Inonga anainua kiatu juu ya Sureboy, inapulizwa filimbi na zogo linatokea

45+4' 🟨Sureboy anapewa kadi ya njano kwa kumletea ubabe Inonga

45+4' 🟨Inonga anapewa kadi ya njano kwa kumchezea ndivyo sivyo Abubakar Sureboy

49' ⚽ Mayeleeee anafanikiwa kutetema mapemaa kipindi cha pili, Yanga 1-1 Simba

55' Sakho anaachia mkwaju na kumgonga Dickson Job, mkwaju wa kona wa Simba unashindwa kubadili matokeo

57' Morisson na Ki wanacheza gonga langoni kwa Simba lakini beki wa Simba anatbua mipango

59' Inonga yuko chini baada ya kukwatuana na Aziz Ki

59' SUB: Simba wanafanya mabadiliko, Mzamiru na Okra wanaingia, Chama na Kanoute wanaenda nje

65' Yanga wanasaidiwa na mtambaa wa panya kuokoa mpira, jaribio zuri kwa Simba SC

69' SUB: 'Mzungu wa Simba' Dejan Georgijevićanaingia kuchukua nafasi ya Habib Kyombo

70' Almanusura Fiston aandikishe bao la pili, Quatarra anaweka mguu na kuhamisha mpira

72' Mayele anaukosa mpira, pasi ya wazi kutoka kwa Aziz Ki

78' Simba wanapata kona ya nne ya mchezo, Quatarra anapiga juuu

80' ⚽ Siku ya Kutetema, Fiston Mayele anaweka tena... Yanga 2-1 Simba

80' Dickson Job alimpa Mayele na Fiston akaachia mkwaju kwenye msitu wa wachezaji watatu wa Simba

83' Mayele anajaribu tena lakini Beno anakaa imara

84' SUB: Makambo Ebenezer anaingia kuchukua nafasi ya Fiston Mayele. Upande wa Simba Bocco anaingia

89' Morisson anaachia mkwaju unaopanguliwa na Beno Kakolaya

90+4' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwisho wa mchezo. Mayele anawalaza na viatu Simba SC

Yanga SC anatwaa ngao ya Jamii na pazia la ligi kuu linafunguliwa rasmi. Yanga 2-1 Simba


=========


Tarehe imewadia.
Klabu mbili kubwa hapa nchini zinaenda kukiwasha uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana walipokutana kwenye ngao ya jamii Yanga alipata ushindi wa goli moja lililofungwa na Fiston Mayele.

Je, mnyama mkali atalipiza kisasi au Yanga ataendeleza ubabe? Tutakuwa hapa kupeana taarifa.

Mchezo utaanza saa moja kamili jioni.

=============
Timu zote zimeshawasili Uwanja wa Mkapa.

Kikosi cha Simba
FaDK0Y1XwAAKptd.jpg

Kikosi cha Yanga cha leo
FaDMeMYXwAIVEJ1.jpg

Timu zilipokuwa zikiingia uwanjani mapema leo:
FaDLq2MWQAMs7mq.jpg

FaDC_fsWIAE-TAP.jpg

 
Simba SC imeimarika, kikosi kimebadilika sana kwa kuongezwa wachezaji wenye quality ya uhakika maeneo yaliyoonekana kuwa na upungufu msimu uliopita.

Naamini kabisa mwalimu ameshakijua vizuri kikosi chake, anajua nani anastahili kuanza kwa nafasi yake, muhimu mpira uchezwe uwanjani, yale mambo ya kukanyagana yasiwepo ili tuuone ubora wa kila timu.
 
Tarehe imewadia.

Klabu mbili kubwa hapa nchini zinaenda kukiwasha uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana walipokutana kwenye ngao ya jamii Yanga alipata ushindi wa goli moja lililofungwa na Fiston Mayele.

Je mnyama mkali atalipiza kisasi au Yanga ataendeleza ubabe? Tutakuwa hapa kupeana taarifa.
Simba imepakatwa mapema sana
 
Tarehe imewadia.

Klabu mbili kubwa hapa nchini zinaenda kukiwasha uwanja wa Mkapa Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana walipokutana kwenye ngao ya jamii Yanga alipata ushindi wa goli moja lililofungwa na Fiston Mayele.

Je mnyama mkali atalipiza kisasi au Yanga ataendeleza ubabe? Tutakuwa hapa kupeana taarifa.
Kila la kheri timu langu la yanga
 
Back
Top Bottom