Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wameendeleza kasi yao katika msimu mpya baada ya kuichapa Coastal Union mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex.
Yanga ilionyesha kiwango bora katika mchezo huo na kutumia vyema nafasi ilizozipata mbele ya lango la Coastal Union, huku ikifanikiwa kupata mabao manne yaliyowekwa kimiani na Kagwanda, Max Mpia, Mudathir Yahya na Mohamed Hussen.
==================
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans Sports Club (Yanga), leo Alhamisi Agosti 20, 2026, wanatarajiwa kushuka dimbani dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 12:30 jioni kwa saa za Tanzania na utachezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na morali baada ya kuanza vizuri msimu kwa kuifunga Namungo FC mabao 3-1 katika mchezo wao wa kwanza wa ligi.
Macho ya mashabiki wa soka Tanzania leo yataelekezwa kwenye mchezo huo, ambao unatarajiwa kutoa picha ya uwezo wa Yanga katika kuanza kampeni yake ya msimu na pia kuonyesha kama Coastal Union inaweza kuwazuia mabingwa hao kupata pointi muhimu.