FT: Yanga S.C 0-0 Rivers United | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 30.04.2023. Yanga yatinga Nusu Fainali

FT: Yanga S.C 0-0 Rivers United | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 30.04.2023. Yanga yatinga Nusu Fainali

Niseme tu wazi nakemea na inaudhi sana mechi ya SAA moja usiku mtu anaanzisha thread mid night, huu ni ujinga kusema ukweli.

Maxence Melo lipokee hili na lifanyiwe kazi ikiwezekana game Kubwa thread ya Live iwe ni jukumu la moderator na thread ya porojo kama hii iachwe kwa ajili ya porojo za mashabiki.

Maana thread ya hivi muda wa mechi ukifika unakuta page kibao hujui uanzie wapi.

Hii tabia inaota mizizi kwenye hili jukwaa ni vizuri ikatafutiwa ufumbuzi, mpaka mtu anaweza kudhani kuna malipo yanatolewa kwa atakayewahi kufunguwa thread ya mechi, huu ni ujinga.
Ubaya ni kuwa wanakimbilia kuanzisha nyuzi na updates hawaleti.

Mechi ya dakika 90 mtu kaleta updates mara 10 tu, Scars huyu mwamba huwa anajitahidi kwa updates..

Hawa wa yanga bure kabisa ananogewa na mechi ama lah speed ya kutype hana.
Kuna watu inakua kama na wewe upo kucheki mechi kwa jinsi walivyo sharp.
 
Yanga itafungwa 1-0, wataenda hadi penati na Yanga atatoka Kwa Penati.
Rekebisha kabla ya hujashambuliwa kama nyuki na Wananchi wasiopenda mambo ya hovyo hovyo.

Kwa matokeo yako haya ya kishirikina, bado Yanga anasonga mbele mkurugenzi.
 
Huenda ikiwa game ngumu kwa Yanga nikiwa na sababu zifuatazo:-

1. Kule Nigeria Yanga tulishinda kwa mbinu tu na sio quality ya wachezaji.

2. River United waliwachukulia Yanga poa, wakarelaxy wakijua watashinda walipopigwa la kwanza wskapanic wakajikuta wanapigwa la pili.

3. Yanga game psychology huenda ikawa cost watacheza kwa kurelaxy ili hali River itakuwa jihadi watapambana kweli kweli maana so psychology iliyowagharimu River kwao ndiyo hiyo huenda ikaigharimu Yanga kwa Mkapa.

Lakini ikiwa Yanga wataingia kwa wakiwa na kumbukumbu ya kulipiza kisasi cha kupigwa nje ndani basi wataibuka na ushindi mnono na kutinga semi final na kuweka historia katika ukanda huu.

Niwatakie Yanga ushindi.
Huu ni uongo [emoji16]

Bado Yanga itashinda tu

1. Umesema Kule Nigeria Yanga ilishinda Kwa mbinu Ila sio quality ya wachezaji. Nitajie wachezaji wa Nigeria walionesha quality kuliko wa Yanga...

2. Unasema Rivers waliwachukulia Yanga poa.. huu ni uongo kumbuka Yanga walishanesha dharau nyingi Kwa Rivers siku ya kupangwa droo Hadi wakashangilia kupangwa na rivers sasa hapo Nani alimchukulia poa mwenzake...

3. Umezungumzia kua physically fit haahhahaa Yanga wapo fit kiakili na kimwili kuliko hao wapopo kumbuka Ile faulo Yao walipiga mshambuliaji anateleza mwenyewe it means n wazito.. rejea tena Yule beki alivokimbizwa na Jesus ducapel Moloko [emoji28]

FAMASIALA NINI !!...

[emoji172][emoji169]
 
Nje ya mada kidogo. Hivi kihistoria waanzilishi wa timu ya simba walikuwa kina nani? Walikuwa watanzania kweli? Ukiachana tu na rangi zao rasmi kuwa haziwakilishi chochote Tanzania ila hata nembo yao hamna popote inapoiwakilisha Tanzania. No wonder wakifikwa na mabaya nchi nzima inakuwa na furaha.
f64a0bfa3af7ba54d73de913a4d3fefe.png
bb59f87d244adfb69145a245979b9248.png
 
Back
Top Bottom