FT: Yanga S.C 0-0 Rivers United | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 30.04.2023. Yanga yatinga Nusu Fainali

FT: Yanga S.C 0-0 Rivers United | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium | 30.04.2023. Yanga yatinga Nusu Fainali

Nje ya mada kidogo. Hivi kihistoria waanzilishi wa timu ya simba walikuwa kina nani? Walikuwa watanzania kweli? Ukiachana tu na rangi zao rasmi kuwa haziwakilishi chochote Tanzania ila hata nembo yao hamna popote inapoiwakilisha Tanzania. No wonder wakifikwa na mabaya nchi nzima inakuwa na furaha.View attachment 2604648View attachment 2604649
Rangi ya Simba umewakosea sana,inawakilisha mavazi ya kilinge Cha Mshana Jr na waganda wote Duniani
 
Ni siku ya kipekee siku ya kihistoria katika soka la nchi yetu ambapo tunaweza kushuhudia timu kutoka Tanzania kwa mara ya kwanza ikitinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Timu hiyo si nyingine Bali ni Mabingwa wa nchi na vikombe vyote nchini na ambao ndio wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki na kati katika michuano ya kimataifa Young Africans almaarufu Yanga.
Leo jioni wanashuka dimbani Estadio de Benjamini Mkapa kumenyana na Rivers United katika hatua ya robo fainali kombe la shirikisho barani Afrika.

Ikumbukwe mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa kule Nigeria, Yanga walipata ushindi wa mabao 2-0, Hivyo wataingia Uwanjani wakiwa na kiu ya kuendeleza ubabe wao mbele ya mapopo na kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Pia Yanga watakuwa na kiu ya kulipa kisasi cha kufungwa na hawa Rivers nje ndani hivyo watakuwa na kila sababu ya kupata ushindi kwenye ardhi ya nyumbani,

Mchezo huu utapigwa mishale ya saa 1.00 usiku na utarushwa na Azam Sports kupitia channel ya ZBC2
View attachment 2604213View attachment 2604214
Yanga anakwenda kucheza fainali za shirikisho Hilo halina mjadala period
 
Niseme tu wazi nakemea na inaudhi sana mechi ya SAA moja usiku mtu anaanzisha thread mid night, huu ni ujinga kusema ukweli.

Maxence Melo lipokee hili na lifanyiwe kazi ikiwezekana game Kubwa thread ya Live iwe ni jukumu la moderator na thread ya porojo kama hii iachwe kwa ajili ya porojo za mashabiki.

Maana thread ya hivi muda wa mechi ukifika unakuta page kibao hujui uanzie wapi.

Hii tabia inaota mizizi kwenye hili jukwaa ni vizuri ikatafutiwa ufumbuzi, mpaka mtu anaweza kudhani kuna malipo yanatolewa kwa atakayewahi kufunguwa thread ya mechi, huu ni ujinga.
Sahih mashindano as if Kuna malipo wanapata
 
Makelele mengi kombe lenyewe la loser.....
IMG_20230429_200940.jpg
 
Kuna mwamba huyo kutoka Naija ana utege hatari, mashuti yake ya ndoige. Mkitolewa leo msifanye vurugu maana mlishaahidi kisasi ni haki. Mtatuletea shida tunaojiandaa kwa super league.
 
Kuna mwamba huyo kutoka Naija ana utege hatari, mashuti yake ya ndoige. Mkitolewa leo msifanye vurugu maana mlishaahidi kisasi ni haki. Mtatuletea shida tunaojiandaa kwa super league.
Wewe muda huu ulitakiwa uwe katika mapokezi ya timu yenu huku kwenye mashindano ya CAF umefuata nini? Kuna timu yako inayoshiriki? Nyie mkae muangaike na Azam Federation na ligi kuu. Huku kwenye CAF msubirie super league na msimu mpya wa CAF mwezi wa 8
 
Mnahitaji baraka za Simba ili mfike huko maana ndiyo timu pekee ya TZ imewahi kukanyaga anga hizo mnazoota kufika. Tambo zenu zitawaponza.
 
Mnahitaji baraka za Simba ili mfike huko maana ndiyo timu pekee ya TZ imewahi kukanyaga anga hizo mnazoota kufika. Tambo zenu zitawaponza.
Kwani mpaka hapo walipofikia Simba imeshatoa baraka gani? Hizi tambo mlizianzia nyie wenyewe mliyojiona watoto wa CAF. Saivi mmeamua kushangilia timu ipi ya CAF baada ya kutolewa?
 
Kwani mpaka hapo walipofikia Simba imeshatoa baraka gani? Hizi tambo mlizianzia nyie wenyewe mliyojiona watoto wa CAF. Saivi mmeamua kushangilia timu ipi ya CAF baada ya kutolewa?
Hao madunduka wasikuchanganye so tunawatambua kama wafa maji Tu.
NA kamwe hawatoacha kutapatapa
 
Back
Top Bottom