FT: Yanga SC 2-0 US Monastir | CAFCC | Benjamin Mkapa | 19.03.2023

FT: Yanga SC 2-0 US Monastir | CAFCC | Benjamin Mkapa | 19.03.2023

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Wananchiiiiiiiiiìiiiiiiiiii
Usiku wa deni haukawii kukuchwa. Leo ndiyo ile siku tuliyoisubiri kwa hamu kwa Yanga kukata tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya CAFCC.

Saa moja jioni mbivu na mbichi kujulikana. Tupo hapa kuisubiri saa 1 jioni ili tumalizane.
Mimi na wenzangu tupo hapa kukupa updates kinachojiri kabla, wakati na baada ya mechi. Usiondoke.

20230319_191503.jpg

Kikosi cha Yanga

Mchezo umeanza licha ya mvua kubwa kinyesha Dar es Salaam
2' Mayele anapiga shuti kali nje ya 18 kipa anapangua
5' Yanga wanatawala mchezo
10' Presha ni kubwa kwa wageni
16' Djuma Shaban anapiga shuti kali nje ya 18 kipa anapangua inakuwa Kona
19' Yanga wanapata Kona nyingine
20' Monastir wanajaribu kujipanga lakini presha inakuwa kubwa kwao
Gooooooooooo
33' Musonda anaipatia Yanga goli la Kwanza kwa kichwa
39' Aucho anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
Musonda.jpg
45' Mapumziko

Kipindi cha pili kimeanza
47' Yanga wanagongeana karibu la lango la Monastir lakini mpira unatoka nje
55' Gooooooooooo
Mayele anaipatia Yanga goli la pili kwa shuti kali
64' Yanga wanaongeza presha kwa wapinzani
71' Djuma Shaban wa Yanga anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda
83' Presha ya mchezo imepungua kidogo
83' Anatoka Mayele anaingia Clement Mzize
89' Diarra anapata kadi ya njano kwa kuchelewesha muda
90' Zinaongezwa dakika 4

Full Time
 
IMG_5316.jpg

Mabingwa wa kutandaza soka tamu, soka la kuvutia, soka la kumtoa nyoka pangoni, soka ice cream, soka lenye viwango vya Dunia, hapa nawazungumzia Young Africans leo mida ya saa 1.00 usiku watashuka pale dimba la Benjamini Mkapa kutafuta alama tatu zingine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia robo fainali ya michuano ya shirikisho barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa mchezo wa awali uliopigwa huko nchini TUNISIA [emoji1249] timu ya US MONASTIR iliichakaza vibaya sana wananchi kwa kuwafunga 2-0 hivyo mchezo wa leo utakuwa mkali kwa timu zote. Yanga anahitaji ushindi ili afuzu robo fainali kwa mara ya kwanza
 
View attachment 2557449

Mshana Jr njoo uweke baraka zako hapa
 
Mods kwa nini mnaruhusu huyu mamluki kuanzisha uzi huu? Alianza kuanzisha Uzi wa kushabikia timu pinzani, ina maana atakuwa analeta up dates za upande mmoja tu.
Pole Sana Changamoto
Mrunga Mbunga Ni Ngumi Mpya Karim Matonga Mtu Kazi Toka Jangwa La Sahara
 
Back
Top Bottom