View attachment 2557449
Mabingwa wa kutandaza soka tamu, soka la kuvutia, soka la kumtoa nyoka pangoni, soka ice cream, soka lenye viwango vya Dunia, hapa nawazungumzia Young Africans leo mida ya saa 1.00 usiku watashuka pale dimba la Benjamini Mkapa kutafuta alama tatu zingine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuingia robo fainali ya michuano ya shirikisho barani Afrika.
Ikumbukwe kuwa mchezo wa awali uliopigwa huko nchini TUNISIA [emoji1249] timu ya US MONASTIR iliichakaza vibaya sana wananchi kwa kuwafunga 2-0 hivyo mchezo wa leo utakuwa mkali kwa timu zote. Yanga anahitaji ushindi ili afuzu robo fainali kwa mara ya kwanza