Fuata moyo wako lakini usisahau kubeba akili yako

Mada nimeikimbilia nikajua ni pana. kumbe umeifinya kwenye mapenzi tu.

Huko kwenye maisha mengine kama biashara, maamuzi kazini nk.
 
Umenena vema kabisa
 
Malizia tujifunze kitu mkuu
Nilikuwa na huu mpango sema nimeona kama nitatoka nje ya lengo la mleta mada, ndio maana nikataka amalizie mwenyewe ili nisiharibu mtiririko wake wa mawazo.

NB. Haya maisha tunayoishi especially kwa waliomaliza vyuo wengi huwa na ndoto zao [wakisikiliza mioyo yao], bahati mbaya pressure wanayoipata toka kwa members wa familly huwakatisha tamaa kufuata mioyo yao hivyo kuwachelewesha kuyafikia malengo yao, wakiendelea kukaa tu home kusubiri ajira huku miaka ikienda.

Makazini napo, wengi huwa wanapenda kujiendeleza kimasomo, au wengine kuacha kazi wafanye kitu kingine [wote hawa husikiliza mioyo yao]. Lakini wengi wao huchukua muda sana kutimiza malengo yao hasa wakiwashirikisha watu wengine mipango yao.

Vyema hawa watu wafuate mioyo yao kwenye kufanya kile wapendacho, lakini wawe na akili ya kuchambua mbivu na mbichi wanazoshauriwa wa walioko karibu nao, ndio maana mleta mada anasema fuata moyo ila usiache akili yako.
 
Kufuata maamuzi ya moyo kunaleta ari na furaha ya maisha, lakini ni lazima akili iongoze hatua ili usitumbukie kwenye majanga.

Moyo ni injini inayokusukuma kutafuta mabadiliko kimasomo au kikazi na hata kimaisha, ilihali akili ni usukani unaokuepusha kugonga miamba ya kiuchumi na kijamii.

Unapoweka siri mipango yako, unaruhusu shauku ya moyo wako ijenge ndoto kubwa, huku ukitumia akili yako kufanya tathmini ya hatari na kuandaa akiba ya dharura.

Maisha yenye mafanikio yanahitaji usawa huu...!
moyo unaamua mwelekeo utakaokupa amani, lakini akili inatengeneza ramani thabiti ya kiutendaji inayofanya ndoto hiyo kuwa kweli bila kutegemea maoni ya nje.

 
Nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…