Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,298
- 3,059
Ni hotuba nzuri na kwa wakati muafaka, hongera Mh. Mbowe!
Ni wakati sasa viongozi na Serikali wathamini uhai na maisha ya Watanzania kuliko vitu na siasa. Uchumi sio kipimo pekee cha kujenga hoja za hatua stahiki za kuchukua kipindi hiki. Maana mpaka sasa biashara nyingi zimedorora na kuathiri uchumi (hasa wa mtu mmoja mmoja na kaya). Pia kulinda maslahi za kisiasa kama umaarufu nk sio kigezo sahihi mbele ya uhai na maisha ya Watanzania.
Ni kweli kuwa mpaka sasa Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika kushughulikia, kuchambua, kutoa taarifa na maamuzi yenye weledi na tija - hasa kwenye leadership & political willness. Hilo halina mjadala. Lakini si vibaya kujifunza pale mtu ulipokosea na kujirekebisha bila aibu wala chenga; kwa hiyo basi muda uliopo utumiwe vizuri ili kurekebisha kasoro na mapungufu yote yaliyojitokeza bila hiana wala vitisho. Natambua kuwa suala la Covid 19 ni tata na gumu, lakini bado ni wajibu wa Serikali yetu (mstari wa mbele) na wananchi mmoja mmoja (mstari wa pili) kuchukua hatua zote za msingi kujilinda wasiambukizwe wala kuambukiza. Mpaka sasa awareness ni ndogo mno miongoni mwa wananchi, hilo ni bomu jingine.
Nikiri wazi kuwa bado sijaelewa hasa msingi na faida ya kuficha-ficha takwimu na hali halisi ya; visa/maambukizi, kupona na vifo vya Covid 19! Maana huko mitaani watu wanazo takwimu "halisi na ngumu" za ndugu na majirani zao wanaougua na kufariki, na wanaougua na kupona; hizo hazichakachuliki na adhari yake ni mbaya na kubwa kuliko kama wangeambiwa ukweli moja kwa moja na Serikali, na ambapo huenda wangechukua tahadhari zaidi. Yaani taharuki ya yanayotokea mitaani ni mbaya (iko out of control) kuliko kama Serikali ingekuwa wazi na shirikishi zaidi.Katika mazingira hayo habari za uvumi & uongo hutamalaki kwa vile umma hauna tabia wala uwezo wa kuthibitisha/kupima unachosikia, badala yake hu react.
Na wauguzi na wafanyakazi wa afya wajengewe uwezo na mazingira ya kutekeleza kazi yao ili kuokoa maisha ya waathirika. Budi tupaze sauti zetu sasa maana historia itatuhukumu, time is always a just judge. Tukosoe na kushauri, tushiriki na kutenda kwa ajili ya uhai wetu, familia zetu, jamii zetu na nchi yetu.
Nimalizie mchango wangu wa mwezi hivi:-
"If you do not plan to succeed then (automatically) you are planning to fail"
"It is never too late to right the wrong"