Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,705
- 4,703
Hili ndo binafsi sihitaji kuliona ktk nchi. wanasiasa kudhania hata mambo ya magonjwa ni kazi yao kutuhutubia. mtu hana sifa anaamua tu kuandika na kuweka signature ya vyeo vya kisiasa ili tuamini ni sawa. Imefikia hatua watanzania ni watu wa kuhutubiwa na yeyote juu ya chochote. Bahati mbaya tunasikiliza kila kitu. Na hakuna asiye na wafuasi.
Mbowe hana sifa za kuzungumzia corona, Magufuli ana sifa hizo kwa nguvu ya kupata taarifa kutoka kwa maafisa wa serikali wanaohusika na taaluma hiyo. Ni vizuri sana wanasiasa watoapo hotuba hizo waandamane na wataalamu kama mganga mkuu wa serikali kujibu na kueleza mambo ya kitaalamu. Kwa ujumla wanasiasa hawana sifa za kuzungumzia undani wa COVID-19. Ifikie hatua kutoa hotuba iwe ni kazi ya wenye taaluma.
COVID ni suala la Kitabibu na siyo kila asiyeweza kukamatwa anatoa hotuba. Tungefurahi kama Chama Cha Madaktari kingetoa msimamo wake juu ya hili, kama limekuwa ni baya kiasi hicho. Lakini kujidai kutuhutubia na kukosoa na kupendekeza, ni kutafuta sifa za kijinga. Eti kiongozi wa kambi ya upinzani, so what?