Full Time: Kagera Sugar 0-2 Simba SC | Ligi Kuu Bara (VPL)

Full Time: Kagera Sugar 0-2 Simba SC | Ligi Kuu Bara (VPL)

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (VPL), kuendelea leo kwa mechi mbili kupigwa.

Baada ya kupigwa 4G na Simba SC uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Singida United leo watakuwa uwanja wa Maji Maji kukipiga na Wanalizombe Majimaji FC, je nani kuibuka mbabe?

Katika dimba la Kaitaba shughuli kuwa pevu wenyeji Kagera Sugar kukipiga na Simba SC. Uwanja wa Kaitaba huwa ni mgumu kwa Simba kupata pointi, je leo atavunja mwiko ama Kagera ataendelea ubabe wake kwa Simba kama ilivyokuwa msimu uliopita?

Kumbuka mechi hii itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2 na kwa upande wa radio TBC Taifa itapeperusha matangazo hayo kuanzia saa 10: 00 jioni hii. Kaa tayari kuletewa mtanange mzima. Usikose ukaambiwa kuwa nasi...!
=================

UPDATES:
Hali ni shwari katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba, huku mashabiki wakianza kuingia tayari kwa kushuhudia mtanange kati ya Kagera Sugar na Simba SC.

1.jpg
2.jpg


Vikosi vya leo tukianza na wenyeji Kagera Sugar;

Juma Kaseja, Eladius Mfulebe, Adeyum Ahmed, Juma Said Nyosso, Mohamed Fakhi, George Kavile, Pastory Athanas, Ally Nassor, Jafary Kibaya, Ally Ramadhan, Atupele Green.

Sub; Ramadhani Chalamanda, Suleimani Mangoma, Peter Mwalyanzi, Juma Shemvuni, Christopher Edward, Paul Ngalyoma, Japhet Makalai.

Na upande wa Simba SC, ambao ni wageni wa mchezo huu;

Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, John Bocco, Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi.

Sub; Emmanuel Mseja, Mohamed Hussein, Mzamir Yassin, Yusufu Mlipili, Shomari Kapombe, Laudit Mavugo, Mwinyi Kazimoto.
======

01' Mpira umeanza na faulo ndogo inatokea baada ya mchezaji wa Kagera kuangushwa.
05' Okwi anaangushwa chini na inakuwa faulo kuelekea Kagera, hata hivyo mpira unapaa juuu ya goli.
08' Kagera wanacheza gonga nzuri kuelekea lango la Simba lakini offside inawaangusha.
10' Kadi ya njano kwa Juma Nyosso
12' Atupele anajaribu bahati yake kutoka mbali lakini mpira unaenda nje ya lango la Simba
15' Kona ya kwanza wanapata Simba lakini inaondoshwa mbali na Kagera.
16' Kagera na wanapata kona na Manula anadaka baada ya shuti kuelekea langoni kwake.
18' Simba wanapata faulo nyingine kuelekea lango la Kagera lakini Kichuya anaubabatiza ukuta wa Kagera.
31' Kagera wanapata kona baada ya Asante Kwasi kutoa mpira nje, Erasto Nyoni anaondoa kwenye lango la hatari.
32' Juma Nyosso yuko sambamba na Okwi kuhakikisha hatembei na mpira.
34' Kadi ya njano kwa Juma Fakhi wa Kagera sukari baada ya kucheza ndivyo sivyo kwa Okwi.
35' Okwi anapiga shuti kali la mpira wa adhabu na kupaa juu kidogo ya goli.
37' Almanusura Jurko Murshid ajifunge katika jitahada za kuokoa, Kagera wanapiga kona kuubwa.
39' John Bocco analamba kadi ya njano na kuwa kadi ya kwanza kwa Simba.
40' John Kavira anaonywa baada ya kumuangusha Okwi, Asante anaunganisha krosi nzuri ya mpira wa adhabu lakini unapita juu ya goli.
42' Ahmed Salehe wa Kagera yuko chini na anatoka nje kutibiwa kisha kurejea.
45+2' Dakika 45 zimekamilika kwa suluhu isiyokuwa na magoli, KAGERA SUGAR 0-0 SIMBA SC.

Kipindi cha pili kimeanza
59' Hakuna goli mpaka sasa
Gooooooool
69' Simba wanapata goli la kwanza la kuongoza
Simba 1, Kagera suger hawajapata kitu

Gooooool

79' John Bocco anaiandikia Simba goli la pili huku akipokea pasi safi kabisa kutoka kwa Shomari Kapombe

Simba 2, Kagera hawajapata kitu.

88' Bado kuna mashambulizi ya pande zote yanaendelea huku simba wakitaka kuongeza bao na Kagera wakijaribu kutafuta bao.

94' mpira utamalizika muda wowote
Okwi anafanya shambulizi almanusra ampige kipa chenga lakini kipa anacheza kwa umahiri kabisa.

Na mpiraaa umekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Kagera 0, Simba 2
 
..Kagera angalieni msitukamie itawakuta kilichowakuta Dijon walipocheza na PSG 8-0
 
Au kilichowakuta Singida United kwa kujifanya wanawaweza Simba sc, kwenye kabumbu.
 
Azam itakuwa mubarasha kuwaletea pia pambano kati ya Juma Nyoso Vs John Boko, usikose kutazama
 
Toka nianze kuishabikia hii timu yangu ya kagera haijawahi kupoteza mchezo siku ya juma tatu hata kutoa suluhu ya aina yoyote ile ni ushindi tu
 
Back
Top Bottom