Full Time: Mwadui FC 2 - 2 Simba SC kutoka dimba la CCM Kambarage, Sinyanga

Full Time: Mwadui FC 2 - 2 Simba SC kutoka dimba la CCM Kambarage, Sinyanga

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Niko hapa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambapo leo timu ya Mwadui FC inamkaribisha mnyama mkali wa mwituni, Simba SC na nitakuwa nakuletea mubashara yale yanayojiri mpaka pale mchuano huu utapoenda kuisha.

Tuwe pamoja kwa updates: Mwadui VS Simba

Kikosi cha Mwadui FC: Anold Massawe, Revocatus Richard, David Luhende, Joram Mgeveke, Iddy Mfaume, Awesu Awesu, Jean-Marie Girukwishaka, Paul Nonga, Evarigestus Mjwahuki, Miraji Athuman.

SUB: Dionis, Malaki, Salum, Matogolo, Rajabu, Mathias, Salvatory.

Kikosi cha Simba SC: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Juuko Murshid, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Emmanuel Okwi, John Bocco, James Kotei.

SUB: Mseja, Ally Shomary, Mavugo, Gyan, Kazimoto, Yassin, Bukaba.

Dimba.jpg

Muonekano wa dimba la CCM Kambarage


01' Mpira umeanza

02' Simba wanaendelea kupandisha mashambulizi kwenye lango la Mwadui

03' Timu zote zina uchu wa kufunga magoli lakini mara nyingi wanajikuta ktk kuotea

04'Mwadui wanashambulia lango la simba kupitia kwa Awesu.

05' Mpaka sasa hakuna shambulizi kali kwani timu zinacheza kwa umakini mkubwa hasa safu za ulinzi.

08'Beki wa Mwadui anatoa boko kwa kumpasia John Bocco mpira anadhibitiwa hapa.

09' Faul inapigwa kwenye lango la Mwadui
Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
John Bocco anaipatia simba goli la kwanza baada ya faul iliyopigwa na Shiza Ramadhani Kichuya na Bocco akaiunganisha kwa kichwa ikajaa moja kwa moja golini.

10'Mpira unachangamka hapa baada ya simba kupata goli la kuongoza, okwi amekuwa naingia ndani lakini anadhibitiwa inakuwa ni kona, kona imepigwa lakini haijakuwa na madhara.

15'Mwadui wanafanya shambulizi lakini wanatoa nje

17'Okwi anambabatiza beki wa mwadui inakuwa ni kona, Kichuya anapiga kona fupi lakini haina madhara.

20' Kona inapigwa kwa mwadui, inatoka nje na inapigwa tena lakini haina madhara

23'Ndemla anapiga krosi lakini inawapita wenzake na kutoka nje.
25' Bocco kaumia na anagangwagangwa
26'Ndemla anapiga faul, kipa anadaka.

27'Mohamed Hussein anaoneshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha mpira

28'Aweso amechezewa faul, faul inapigwa kuelekea lango la Simba.

29'John Bocco anatoka anaingia Mavugo.

31'Faul inapigwa kwenye lango la simba lakini inakuwa haina madhara

32'Miraji athumani anapata nafasi ya wazi baada ya kubakia na kipa lakini anashindwa kufunga.

33'Bocco anapokea shuti lilipigwa kama faul lakini anashindwa kufunga na kujikuta yupo offside.

36' Okwi anapga shuti moja kali lakini kipa analitema.

37'Simba wanaendelea kulisakama lango la Mwadui.

38'Okwi anamchezea beki wa Mwadui faul. Faul inapigwa kwenda lango la simba.

41'Awadhi Juma anapiga shuti kali kuelekea lango la Simba lakini linatoka nje.

44'Simba wanaanzisha tena mashambulizi kwenda lango la Mwadui

45'Kichuya anapiga shuti lakini kipa anaidaka.

45+1' Mwadui wanafanya shambulizi ila wanadhibitiwa

45+3' Mpira ni Mapumziko

Kipindi cha pili
45'Kipinidi cha pili kinaanza.

46' Kapombe anarusha mpira kuelekea Mwadui

50'Mwadui wanaongeza mashambulizi, na sasa wanapiga kona lakini inakuwa haina madadhara.

51'Mwadui wanashambulia lakini wanajikuta wapo offside.

55' Miraji Athumani anafanya shambulizi lakini mabeki wa Simba wanamdhibiti.

56'Paul Nonga ameitoa nje baada ya kupigiwa pasi ndeefu

57'Faul inapigwa lango la simba ni karibu kabisa na 18.

59' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

David Luhende anaipatia Mwadui bao la kusawazisha, baada ya kupiga faul iliyomshinda golikipa Aishi Manula na kuingia moja kwa moja golini.

62' Faul nyingine inapigwa na awesu lakini inakuwa haina madhara

63'Kipa wa Mwadui, Massawe anaoneshwa kadi ya njano baada kudakia nje ya eneo lake.Faulu inapigwa lakini kipa anaipangua na inakuwa kona.

64'Kona inapigwa na inakuwa ni piga nikuge golini na Mwadui wanaokoa, kipa wa Mwadui anagangwa lakini anaamka.

68'Okwi anaangushwa ndani ya 18 na inakuwa ni penalt
70'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Emmanuel Arnold Okwi anaifungia Simba goli la pili baada kupiga kwa mkwaju wa penat.

75' Awesu Ali anaonyeshwa kadi ya njano na anatolewa nje baada ya kujiangusha ndani ya 18.

76'Aishi Manula anaanzisha.

77'Mavugo anafanya shambulizi kali baada ya kupokea pasi kutoka kwa kichuya lakini anakuwa sehemu mbaya.

78'Okwi anafanya shambulizi moja kwa shuti moja kali ambalo halijalenga goli.

79'Awesu Ali anapiga kona moja nzuri inawapita mabeki wa Simba lakini mwadui wenyewe wanaitoa nje.

81'Faul inapigwa kuelekea simba, anaipiga Joram lakini inaondoshwa.

83'Faul inapigwa kwenda Mwadui na kichuya lakini anadaka Anold Massawe.

84'Juuco Mushi anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.Faul inapigwa lakini haina madhara.

87'Mavugo anatoka na anaingia Paul Bukaba

89'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.
Paul Nonga anasawazisha baada ya kupiga kichwa kilichotokana na faul iliyopigwa na kuingia golini.

90+5'Mwamuzi anaudaka mpira na anamaliza.

Mwadui 2, Simba 2
 
Niko hapa uwanja wa CCM Kambarage mkoani shinyanga ambapo leo timu ya Mwadui FC inamkuribisha mnyama mkali mwituni Simba SC na nitakuwa nakuletea mubashara yale yanayojiri mpaka pale mchuano huu utapoenda kuisha.

Tuwe pamoja kwa updates
Hali ikoje hapo
 
Back
Top Bottom