Simba walifanya makosa makubwa 2,,kwanza kuruhusu kufungwa goli nyingi South Africa afu nakutoka bila hata goli 1 la ugenini
Kosa hilo lilisababishwa na kujiamini kulikopitiloza na wachezaji na kocha wao kushindwa kufanya pressing ya nguvu kama walivyofanya leo.
Kosa la pili wamefanya kipindi cha kwanza kwa kupoteza nafasi nyingi Sana walizotengeneza na hivyo kuwa na mzigo mkubwa Sana wa kupanda.
Anyway wametoka kwa heshima,ni kukipanga kwa msimu ujao hasa upande wa beki na washambuliaji wenye akili za kufunga.
Nitoe pongezi in advance kwa Al Ahly ambao bila shaka watakuwa mabingwa msimu huu maana kwenye mashindano haya timu pekee zilizopewa nafasi ya kufika mbali ilikuwa Mamelodi na Simba na tayari zimeaga mashindano.