Full time: Robo fainali Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 3-0 Kaizer Chiefs | Benjamin Mkapa National Stadium - Mei 22, 2021

Full time: Robo fainali Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 3-0 Kaizer Chiefs | Benjamin Mkapa National Stadium - Mei 22, 2021

Tatizo Sister anajua mnaenda hatua inayofuata....

Lakini hivi sasa naona katulia, sijui kuna mtu kama za mashavu kwamba "... usitupige kelele wakati mshatolewa... [emoji1787] "
Hahahaaaa hajui sauzi yalitukuta yapi!
 
Hamna cha kufa kishujaa wala nini,mngekuwa mnajua mpira msingeruhusu magoli yote yale mechi ya kwanza.
Simba wametolewa kishujaa,na juhudi za wachezaji mechi hii zimeonekana,kama utaki acha mwakani Simba itashiriki tena itarekebisha makosa.
Simba nguvu moja.
 
Sijui kwanini kacheza dakika zote 90 (Mugalu)

Sijui kwanini simba walicheza mipira mirefu, sijui kwakweli

Wamekosa nafasi nyingi za wazi wangeweza kufunga ata 6 bila

All in all wamejitahidi. Kipindi kingine tena Inshaallah
Swali la kwanza hilo ndio ntk majibu
 
Samahanini mi sijui Moira
Mfano simba ingefunga mabao tano au sita Leo ndo ingefuzu si ndio?
Yani marudiano yazidi Yale ya swali waliyofungwa?
 
Congrats to the lads.. what a game..what a performance.

Kwa Mkapa panaendelea kubaki moja ya viwanja vigumu sana afrika kwa wageni kupata ushindi.

Pamoja hii game ilikuwa yetu kabisa,sema kama wachezaji walichoka ama kujisahau katika kutafuta idadi ya magoli.



Binafsi nampongeza kila mmoja, hakika Simba inaendelea kuweka bars..
Mkiendelea na hii mind set ya kijinga mtakuwa mnaishia kupongezana kea upuuzi.

Timu iloyokomaa na kujielewa inatafita goli ,ushindi au draw ugenini Ili wafike mbali .Mkienda na huu ujinga msimu ujao mtaishia kujifariji kama saizi.
 
Barcelona ina kitu cha kujifunza kwenye mechi hii kupitia uwezo wa simba iliyoonesha
 
Simba wanaume no matter what, utopolo walijua tunakufa na leo kwa Mkapa, hawana maneno tena kimyaa

Kwa Mkapa hatoki mtu, hiyo ni mark Afrika nzima
 
Katika maisha hangu ya soka kuumia kama hivi imetokea mara chache mnoo haswa ni arsenal kufungwa fainali 2006 ya uefa na barca, ufaransa kufumgwa na Italy world cup 2006..

Kidoogo hapa katikati atletico kupoteza zile fainali za uefa mara 2 mbele ya real madrid.

Na leo hii, aisee leo imeniuma haswaa.. [emoji17]
Pole mkuu ila nakushauri utoke huko Asenali nenda timu nyingine
 
Wewe unataka kuturudisha enzi za Tambwe ili tusote tena kupata fowadi mwingine mimi naona wamuache kwanza azoee mazingira pale Simba
Hapana,kukosa magoli ya wazi sio swala la mpaka azowee ni uwezo wa mchezaji kukosa umakinifu wa akili na unyambulifu wa mwili,Mugalu alivyomzito wa mwili na akili yake ni nzito hivyohivyo.
Simba nguvu moja.
 
Kama hawana mpira mmesonga mbele?
Simba na Mamelod zote hazina mpira, ndomaa zimebaki? Kuna muda mpira una maajabu yake tu, hata zile goli 4 kule South sielewi tulipigwaje, Kizer hana mpira wa maana.
 
Mkiendelea na hii mind set ya kijinga mtakuwa mnaishia kupongezana kea upuuzi.

Timu iloyokomaa na kujielewa inatafita goli ,ushindi au draw ugenini Ili wafike mbali .Mkienda na huu ujinga msimu ujao mtaishia kujifariji kama saizi.
Waulize Mamelod Sundowns kama hayo maneno matupu ni rahisi kutekelezeka.
By the way, nyie muko ligi gani?
 
Aliemsajili Mugalu amrudishe alikomtoa, uchafu alofanya leo hatutaki kuona msimu ujao dahhh!
 
Back
Top Bottom