FULL TIME: Ruvu Shooting 0-7 Simba, Uwanja wa Mkapa, ASFC

FULL TIME: Ruvu Shooting 0-7 Simba, Uwanja wa Mkapa, ASFC

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mchezo umemalizika, Chama anakabidhiwa mpira kwa kufunga hat trick.

Full Time
Zinaongezwa dakika 3 za nyongeza
Dk 90: Simba wanapiga pasi na kuumiliki mchezo.
Dk 87: Mchezo umepungua kasi, Ruvu ni kama wamekata tamaa.
Dk 82: Kocha wa Ruvu, Charles Mkwasa anaonekana kuwa katika masikitiko.
Dk 80: Ruvu wanacheza kwa kasi ndogo.
Dk 76: Kipa wa Ruvu, Nitoko anamchezea faulo Mwanuke, inakuwa faulo kuelekea Ruvu.
Chama anafunga bao la saba na la tatu kwake katika mchezo huu.
Dk 72: Goooooooooooooooooo
Dk 70: Jimmy Mwanuke anapata pasi nzuri kutokw kwa Chama na kufunga bao la sita.
Gòoooooooooooooooo
Dk 67: Simba wanapanga mashambulizo taratibu.
Dk 65: Ruvu wanapata faulo nje ya 18 lakini wanashindwa kutumia vizuri.
Dk 60: Simba wamepunguza kasi ya kushambulia na hiyo inawapa nafasi Ruvu kufika langoni kwa Simba.
Dk 55: Ruvu wanatengeneza nafasi kadhaa lakini wanakosa umakini katika umaliziaji.
Dk 50: Simba wanautuliza mchezo
Dk 48: Ruvu wameanza kwa kutulia tofauti na kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili kimeanza.

Mapumziko: Simba wanaongoza kwa mabao 5-0
Gooooooo, Ruvu Shooting wanajifunga.
Dk 42: Mambo ni magumu kwa Ruvu
John Bocco anafunga bao la nne kwa Simba.
Dk 39: Goooooooooo
Dk 27: Chama anaipatia Simba bao la tatu.
Dk 26: Ruvu ni kama wanapoteana.
Dk 25: Chama anaipatia Simba bao la pili baada ya kuwapindua mabeki wa Ruvu.
Dk 12: Ruvu wameamka na kuanza kujipanga, wanafanya shambulizi kali inakiwa kona.
Dk 5: Simba wanafanya shambulizi kali.
John Bocco anaipatia Simba bao la mapema
Dk 2: Goooooooooo
Dk 1: Simba wanaanza kwa kasi
Mchezo umeanza

Mchezo unatarajiwa kuanza saa 1:00 Usiku.

Simba wameshatangaza kikosi chao kwa ajili ya kuivaa Ruvu Shooting katika mchezo wa Raundi ya Tano ya Azam Sports Federation Cup kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

simbasctanzania_164502455972192.jpg
 
Back
Top Bottom