Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Full Time: Simba SC 2-1 CS Sfaxien | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa National Stadium | Disemba 15,2024

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
Leo ndio leo kwenye kipute hiki cha Kombe la Shirikisho Africa kati ya wenyeji Simba ya Tanzania na wageni Sfaxien ya Tunisia.

Hii ni Match Day 3 kwa timu hizi na mechi zilizopita wote walichezea kichapo ugenini (2-1 na 3-2). Leo kila mmoja anatafuta ushindi kufufua matumaini ya hatua ya makundi.

Mechi hii itapigwa saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nini kitatokea katika Dimba la Benjamin Mkapa leo? Kuwa nami mwanzo hadi mwisho wa mchezo huu kupitia JamiiForums.

Azam na DStv pia watarusha mechi hii.
IMG_1585.jpeg

---------------------------------------------
Updates : 1500 Hours Vikosi vya leo
IMG_1628.jpeg
IMG_1632.jpeg

________________________________________________

1' Mpira umeanza kwa Simba kuanzisha mpira hapa... wanashambulia lango la Sfaxien lakini Zimbwe anapiga pasi kuuubwa inaenda nje

2' Goooaaaal Sfaxien wanapata goal hapa kupitia Hazem Hassen

06' Simba wanashambulia hapa Kibu Denis anaangushwa... Freekick inapigwa na Jean Ahoua.. Kibu anafungaaaaa goal 1-1

09' Simba wametulia wanafanya shambulizi la Kushtukiza lakini Sfaxien wanaokoa shambulizi hilo

14' Simba wanamiliki mpira kwa Kiasi kikubwa kwa chenga za hapa na pale wanajaribu kuingia lakini mpira unatolewa nje

19' Musa Conte anamdondosha Awesu Awesu na Simba anapata freekick, Jean Ahoua anapiga ndefu ila kipa wa Sfaxien, Dahmen anaidaka

24' Kapombe anapress kuelekea Sfaxien anampasia Ateba lakini control yake inakuwa sio nzuri anadhibitiwa na mabeki wa Sfaxien matokeo bado ni 1-1

29' Kapombe anachezewa faulo hapa inakuwa ni freekick nje kidogo ya 18.. Kibu anapiga inagonga ukuta, Zimbwe anaiwahi lakini anapiga inatoka nje

33' Ateba na Kapombe wanaonana vyema kushambulia Sfaxien, wanakwenda pale inamiminwa Cross lakini Jean Charles Ahoua anakosa umakini anapaisha juu

38' Sfaxien wanatibua jaribio la Simba mpira unakwenda nje, Simba wanatawala Dimba ila Sfaxien wanakuwa makini

43' Sfaxien wanaachia kombora kali hapa kuelekea langoni kwa Simba ila Camara analipangua na Zimbwe anaokoa

45' Zimeongezwa dakika 5 kuelekea Mapumziko, timu zinashambuliana kwa zamu (1-1)

45+5' Afisa mmoja wa Sfaxien anaoneshwa kadi ya njano..
Halftime... Ni mapumziko SSC 1 - CSS 1

Updates 1707 Hours

46' Kipindi cha pili kimeanza hapa, Ateba nje.. Mukwala kaingia

50' Kibu Denis anashambulia kwenda Sfaxien, anaingia kwenye 18 anaanguka refa anamwambia nyanyuka, no penalty

57' Kadi ya njano kwa Che Malone baada ya kucheza faulo, free kick inapigwa na sfaxien lakini inatoka nje

62' Haboub anaoneshwa kadi ya njano kwa kumzuia Musa Camara kuanzisha goal kick

64' Sub kwa Simba
Mutale
Chamou
Kagoma... Hawa wanaingia

Ahoua Jean
Che Malone
Mavambo Debora ... Hawa wanatoka

66' Steve Mukwala anapiga shuti moja kali mpira unaokolewa na Kipa inakuwa kona... Kipa analala chini kwa maumivu, anatibiwa.. Kona inapigwa na Mutale simba wanaicheza kona tena mabeki wanaokoa, Zimbwe anaitoa nje.. Goal kick

70' Sub kwa Sfaxien

Sekouhi anatoka anaingia Traore Boubacar
Daouhi nje na Becha Yusuf ndani
1-1 bado ndio matokeo

77' Sub kwa Simba

Nouma Valentin anaingia kuchukua nafasi ya Mohamed Hussein

79' Kibu anaangushwa baada ya kupress , inapigwa faulo na Nouma kipa anapangua na mabeki wanaokoa shambulizi lile

84' Simba wanaonana vizuri kuelekea Sfaxien kwa pasi fupi fupi, Wanakosa chance ya goal hapa inapigwa kona Hamza Abdulrazak anaitoa nje kwa kichwa.. Goal kick

88' Simba wabashambulia, inatolewa nje ..inarushwa kuelekea SFAXIEN namna gani pale shuti la Kapombe wa Simba linaokololewa.. Kona.. Inapigwa fupi nayo inaokolewa...

90' Dakika 7 za nyongeza kuelekea Full time

90+3' Joshua Mutale anakosa utulivu anatoa mpira nje kwa shambulizi ambalo angetulia wangepata goal

90+6' Simba wanashambulia hapa wanapata kona inapigwa inaokolewa kona tena

Kona inapigwa lakini Simba wanautoa nje

90+8' Goooooalll Simba wanapata kupitia Kibu Denis

90+9' Mpira umeisha SIMBA SC 2 CS SFAXIEN 1
 
𝗟𝗲𝗼 𝗻𝗱𝗶𝗼 𝗹𝗲𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗸𝗶𝗽𝘂𝘁𝗲 𝗵𝗶𝗸𝗶 𝗰𝗵𝗮 𝗞𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗹𝗮 𝗦𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗰𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝗪𝗲𝗻𝘆𝗲𝗷𝗶 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 𝘆𝗮 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗪𝗮𝗴𝗲𝗻𝗶 𝗦𝗳𝗮𝘅𝗶𝗲𝗻 𝘆𝗮 𝗧𝘂𝗻𝗶𝘀𝗶𝗮

𝗛𝗶𝗶 𝗻𝗶 𝗠𝗮𝘁𝗰𝗵 𝗗𝗮𝘆 3 𝗸𝘄𝗮 𝗵𝗶𝘇𝗶 𝘁𝗶𝗺𝘂 𝘇𝗮 𝗹𝗲𝗼 𝗻𝗮 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝘇𝗶𝗹𝗶𝘇𝗼𝗽𝗶𝘁𝗮 𝘄𝗼𝘁𝗲 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗰𝗵𝗲𝘇𝗲𝗮 𝗸𝗶𝗰𝗵𝗮𝗽𝗼 𝘂𝗴𝗲𝗻𝗶𝗻𝗶 (2-1 𝗻𝗮 3-2) 𝗸𝘄𝗮 𝗵𝗶𝘆𝗼 𝗹𝗲𝗼 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗮𝗻𝗮𝘁𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝗽𝗮 𝗸𝘂𝗳𝘂𝗳𝘂𝗸𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗺𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗺𝗮𝗶𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗸𝘂𝗻𝗱𝗶

𝗠𝗲𝗰𝗵𝗶 𝗵𝗶𝗶 𝗶𝘁𝗮𝗽𝗶𝗴𝘄𝗮 𝘀𝗮𝗮 10 𝗷𝗶𝗼𝗻𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝘀𝗮𝗮 𝘇𝗮 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗸𝗮 𝗠𝗮𝘀𝗵𝗮𝗿𝗶𝗸𝗶

𝗡𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗶𝘁𝗮𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗗𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗹𝗮 𝗕𝗲𝗻𝗷𝗮𝗺𝗶𝗻 𝗠𝗸𝗮𝗽𝗮 𝗹𝗲𝗼? 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮𝗺𝗶 𝗺𝘄𝗮𝗻𝘇𝗼, 𝗸𝗮𝘁𝗶 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗱𝗶 𝗺𝘄𝗶𝘀𝗵𝗼 𝘄𝗮 𝗺𝗰𝗵𝗲𝘇𝗼 𝗵𝘂𝘂 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗵𝗮𝗽𝗮 𝗝𝗮𝗺𝗶𝗶𝗙𝗼𝗿𝘂𝗺𝘀

𝗔𝘇𝗮𝗺 𝗻𝗮 𝗗𝘀𝘁𝘃 𝗽𝗶𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗮𝗿𝘂𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝗵𝗶𝗶
Simba anashinda 4 moja, mapema tu

Ubaya ubwela
 
Hongereni watani kunusulika liwa mara ya nne mfululizo msisahau kuja na maudongo ya mama kumletea my wenu anawasubiri juzi kamnyoosha Azam huku
 
Attachments

  • IMG-20241213-WA0004.jpg
    IMG-20241213-WA0004.jpg
    34.2 KB · Views: 4
CS Sfaxien au kwa kifupi CSS, ni klabu ya soka ya Tunisia yenye makao yake makuu mjini Sfax.

Ni Klabu kongwe ilianzishwa mnamo mwaka 1928. Na rangi zake rasmi za uzi wao (kit / Jersey) ni nyeusi na nyeupe. Uwanja wao wa nyumbani, Taieb Mhiri Stadium, una uwezo wa kuchukua watazamaji 12,000. Jina la utani la kujimwambafai ni Juventus ya Uarabuni (Juventus El Arab ). Kocha mkuu ni Alexander Santos.

View: https://m.youtube.com/watch?v=SeRwFUMWF88
 
𝗟𝗲𝗼 𝗻𝗱𝗶𝗼 𝗹𝗲𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗸𝗶𝗽𝘂𝘁𝗲 𝗵𝗶𝗸𝗶 𝗰𝗵𝗮 𝗞𝗼𝗺𝗯𝗲 𝗹𝗮 𝗦𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗶𝘀𝗵𝗼 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗰𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶 𝘆𝗮 𝗪𝗲𝗻𝘆𝗲𝗷𝗶 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 𝘆𝗮 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗪𝗮𝗴𝗲𝗻𝗶 𝗦𝗳𝗮𝘅𝗶𝗲𝗻 𝘆𝗮 𝗧𝘂𝗻𝗶𝘀𝗶𝗮

𝗛𝗶𝗶 𝗻𝗶 𝗠𝗮𝘁𝗰𝗵 𝗗𝗮𝘆 3 𝗸𝘄𝗮 𝗵𝗶𝘇𝗶 𝘁𝗶𝗺𝘂 𝘇𝗮 𝗹𝗲𝗼 𝗻𝗮 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝘇𝗶𝗹𝗶𝘇𝗼𝗽𝗶𝘁𝗮 𝘄𝗼𝘁𝗲 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗰𝗵𝗲𝘇𝗲𝗮 𝗸𝗶𝗰𝗵𝗮𝗽𝗼 𝘂𝗴𝗲𝗻𝗶𝗻𝗶 (2-1 𝗻𝗮 3-2) 𝗸𝘄𝗮 𝗵𝗶𝘆𝗼 𝗹𝗲𝗼 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗮𝗻𝗮𝘁𝗮𝗳𝘂𝘁𝗮 𝗽𝗮 𝗸𝘂𝗳𝘂𝗳𝘂𝗸𝗶𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗺𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗮𝘁𝘂𝗺𝗮𝗶𝗻𝗶 𝘆𝗮 𝗵𝗮𝘁𝘂𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝗸𝘂𝗻𝗱𝗶

𝗠𝗲𝗰𝗵𝗶 𝗵𝗶𝗶 𝗶𝘁𝗮𝗽𝗶𝗴𝘄𝗮 𝘀𝗮𝗮 10 𝗷𝗶𝗼𝗻𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝘀𝗮𝗮 𝘇𝗮 𝗔𝗳𝗿𝗶𝗸𝗮 𝗠𝗮𝘀𝗵𝗮𝗿𝗶𝗸𝗶

𝗡𝗶𝗻𝗶 𝗸𝗶𝘁𝗮𝘁𝗼𝗸𝗲𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗗𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗹𝗮 𝗕𝗲𝗻𝗷𝗮𝗺𝗶𝗻 𝗠𝗸𝗮𝗽𝗮 𝗹𝗲𝗼? 𝗞𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮𝗺𝗶 𝗺𝘄𝗮𝗻𝘇𝗼, 𝗸𝗮𝘁𝗶 𝗻𝗮 𝗵𝗮𝗱𝗶 𝗺𝘄𝗶𝘀𝗵𝗼 𝘄𝗮 𝗺𝗰𝗵𝗲𝘇𝗼 𝗵𝘂𝘂 𝗸𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝗵𝗮𝗽𝗮 𝗝𝗮𝗺𝗶𝗶𝗙𝗼𝗿𝘂𝗺𝘀

𝗔𝘇𝗮𝗺 𝗻𝗮 𝗗𝘀𝘁𝘃 𝗽𝗶𝗮 𝘄𝗮𝘁𝗮𝗿𝘂𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗲𝗰𝗵𝗶 𝗵𝗶𝗶
Jose katika ubora wako mtani
 
Utopolo mmeanza ujinga wenu
 
Muda wa gemu ukifika wala usijisumbue kutoa updates, haya mashindano ya akina mama hayana maana.
 
Back
Top Bottom