FULL TIME: Singida Black Stars FC 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Liti Stadium | 28.12.2024

FULL TIME: Singida Black Stars FC 0-1 Simba SC | NBC Premier League | Liti Stadium | 28.12.2024

Tembosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,487
Reaction score
3,978
Mtanange mkali Leo.

Kinyanganyiro: Ligi Kuu Tanzania Bara - NBC
Mwenyeji: Singida Black Stars ya Singida
Vs
Mgeni : Simba SC ya Dar es salaam

Uwanja: CCM Liti Singida.

Muda : Saa 10Jioni.
20241228_140008.jpg


Tukutane saa 10 Jioni kwa Maelezo ya mchezo huu.

VIKOSI VYA LEO.
20241228_154238.jpg

20241228_154244.jpg


Updates...

00' Mpira umeanza sasa Simba wameelekeza mpira kwa Singida, wanacheza faulo, inapigwa inaokoloewa.

02' Singida wanacheza rafu wanamzonga refa hapa.
Free kick inapigwa na Ahoua inaokolewa na Beki wa Singida.

05' Simba wanaumiliki mpira kwa asilimia kubwa, wanaonana vizuri, kiungo imekaa sawa.

06' Simba wanafanya shambulizi moja zuri Kipa wa Singida anakaa vizuri. anaokoa.

09' Simba wanafanya shambulizi jingine, inakuwa kona.
Simba wanapata kona ya kwanza inapigwa haileti madhara kwa Singida Black Stars.
Mpira unaendelea.

13' Mpira umesimama kwa muda kidogo.
Kipa wa Singida Black Stars anapatiwa matibabu hapa.

18' Tchakei wa Singida Black Stars anapewa Kadi ya njano kwa kumzonga mshika kibendera.

22' Singida Black Stars wanapata kadi nyingine ya njano, Emoro kwa kucheza rafu. Wanapata free kick Simba inapigwa haileti madhara.

23' Metacha yupo chini tena, akitibiwa mpira umesimama kidogo hapa Matokeo bado ni
0-0

30' Singida Black Stars wanapata kona, inapigwa haileti impact yoyote kwa Simba.

32' Simba wanapoteza nafasi ya wazi kabisa hapa.
Inakuwa off target. Mukwala alikuwa na nafasi yakufunga hapa, labda uwezo mdogo.

33' Singida Black Stars wanapata free kick nje kidogo ya 18, inapigwa simba wanakataa.
Mpira Unaendelea
0-0

36' Rupia wa Singida Black Stars anàpoteza nafasi ya wazi kabisa hapa. Anafanya shambulizi ambalo linaishia kuwa goal kick.
0-0

41' Simba wanapata kona inapigwa na Ahoua
Ngomaaaaa Goooooooooooal.
Simba wanatangulia kwa Goli la Ngoma.
0-1

44' Kibu D anapiga tick taka moja matata sana, inakuwa off target.
0-1.

45' Zimeongezwa dakika 4.
0-1

45+2' Camara anafanya save nzuri sana.
0-1

HT
0-1

*************************
Kipindi cha Pili.

46' Rupia anadakwa kwenye eneo la kuotea.
Mpira unaendelea
0-1

47' Singida Black Stars wanapata free kick nje kidogo ya 18 wanapiga haileti madhara.

48' Rupiaaa anapiga shuti kali linaishia kwenye mikono ya Camara kipa wa Simba.

Ngoma anachezewa faulo inakuwa free kick upande wa kulia wa goli la Singida, inapigwa kipa anaitoa Kibu anamsukuma Kipa, Mpira unaingia wavuni, refa anakataa.

51' Ngoma anachezewa faulo tena.
Watu wa huduma ya kwanza wanaitwa, Ngoma ananyanyuka.
Anapiga free kick Ahoua inakataliwa na Wachezaji wa Singida.
Mpira Unaendelea
0-1

58' Kennedy Juma anapewa yellow card kwa kumzonga mwamuzi.
0-1

61' kuna tokea maamuzi ya utata hapa.
Singida Black Stars wanachezewa rafu lakini refa anasema mpira uelekee kwao. Pengine ni kwasababu mchezaji wa Singida Black Stars waliushika

63' Sub
Singida Black Stars
Lyanga Inn
Tchakei Out
Inyama Inn
Imoro Out.
Mpira unaendelea
0-1

64' Mukwala anatoa pasi kwa Ahoua anaipiga vizuri Metacha anakataa.
Inakuwa kona ya Nne kwa Simba.
Anaipiga Ahoua inaokolewa na SBS.
0-1

65' Yusuf Kagoma wa Simba anapewa yellow card kwa kumchezea Rafu Lyanga.
Mpira unaendelea
0-1

66' Wachezaji wawili wa Singida Black Stars wako chini mpira umesimama kidogo hapa.
0-1

70' Mabadiliko kwa Simba.
Mohamed Hussein Out
Chamou Inn
Elia Mpanzu Out
Aweso Aweso Inn
Mpira unaendelea sasa
0-1

75' Mabadiliko Kwa Singida Black Stars
Gego Out
Adebayoh Inn
Mpira unaendelea
0-1

79' Ahoua yuko chini na kitanda cha wagonjwa kimeingia kumtoa nje.
Nafasi yake inachukuliwa na Debora Mavambo Fernandes.
Mpira unaendelea
0-1

87' Simba wanapata Free kick inapigwa na Kagoma, inakuwa goal kick.
0-1

90+1' Mabadiliko kwa Simba.
Ateba Inn
Mukwala Out.
Dakika za Nyongeza ni 3.
Mpira unaendelea
0-1

FT
Singida Black Stars 0 - 1 Simba SC
 
Back
Top Bottom