Ngao ya Jamii: Alhamis hii ni nusu fainali ya wababe. Saa 1:00 usiku ni Kariakoo Derby Yanga SC dhidi ya Simba SC ngoma itapigwa dimba la Benjamin Mkapa.
Dakika 2, Mpira umeanza kwa kasi sana.
Dakika 4, Yanga wamekosa nafasi ya wazi baada ya Prince Dube kupiga mpira ukagonga nguzo ya goli.
Dakika 6, Steve Mkwala anakosa nafasi ya wazi kuweka mpira kimiani.
Dakika 11, Yanga wanatengeneza nafasi nzuri ila wameshindwa kuitumia vyema.
Dakika 17, Timu zote zinacheza kwa tahadhari sana kila mmoja anafanya mashambulizi ya kushutukiza.
Dakika 22, Simba wameendelea kumiliki mpira
Dakika 24, Simba wamepata faulo ila wanashindwa kuitumia vyema.
Dakika 26, Max Mpia anakosa nafasi nzuri kabisa.
Dakika 30, Simba wamekuwa wa moto sana wakiendelea kupima watu umri.
Dakika 32, Yanga wanapata faulo tuone kama watafanikiwa kuweka mpira wavuni.
Dakika 33, Yanga wanakosa faulo waliyoipiga.
Dakika 36, Yanga wamekuwa watulivu sana wanaendelea kutengeneza nafasi.
Dakika 37, Aucho anapata kadi ya njano baada ya kumfanyia mazambi Steve Mutala.
Dakika 41, Aziz ki anakosa nafasi ya wazi baada ya kupiga shuti zito na mpira ukapenda kutoka nje.
Dakika 43, Max Mpia anakosa nafasi nzuri baada ya kupewa pasi nzuri na Aziz Ki
Dakika 44, Max anawapa goli hapa Yanga gooooooool
DAkika 45, Yanga 1-Simba0
Dakika 45 za Kipindi cha Kwanza zimetamatika Yanga SC 1- Simba SC 0
Kipindi cha pili kimeanza na Yanga wanafanya mabadiliko ya anaingia Mzize anatoka Prince Dube.
Simba Pia wanafanya mabadiliko anatoka Mzamiru anaingia Oka Jefa.
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi sana kwa timu zote mbili.
Dakika 44, Simba wamepata koni 3 dotto zote wamekosa kuzitumia vyema.
Dakika 59, Bado shughuli nzito Yanga wanaendelea kuongeza goli la pili nao Simba wanapambana kurudisha