Fundi Niyonzima sasa rasmi Simba SC, hongera mtani

Fundi Niyonzima sasa rasmi Simba SC, hongera mtani

Bora aende zake! Ametusaidia kiasi cha kutosha ila kama simba wamempa pesa nzuri ni jambo jema! Yanga ilikuwepo, ipo na itakuwepo! Ngoja tuomboleze kwanza msiba wa Alli Yanga!

Sizitaki MBICHI hizi..MPIRA biashara mdogo wangu...
 
Habari iliyovunjikavunjika ninayoweza kuwapeni kwa sasa.

Haruna Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia Simba. Yanga wameshindwa kumshawishi Niyonzima abaki kwa kuwa fedha aliyoitaka wameshindwa kumpa.

======

TAARIFA KWA UMMA

Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa inapenda kuwajulisha wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga juu Mchezaji raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye amekua Mchezaji wetu kwa misimu 6 mfululizo katika kiwango cha juu.

Hata hivyo Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hatutaweza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwani hatukuweza kufikia mwafaka katika mazungumzo yetu na yeye licha ya timu yetu kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.

Klabu inamtakia kila la kheri katika maisha yake na soka kwa ujumla.

Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Young Africans Sports club.
21-06-2017.
Safi sana Yanga hii ndio yanga ninayoijua hakunaga kuremba
 
Kila la kheri, ana uwezo mkubwa ila sio waku demand 70/= Milioni.....
Mkuu ilikuwepo hiyo m 70,mwisho wa siku akapandisha m 120,juzi usiku ndio uongozi ulipong`amua alishasaini upande wa pili muda sana,alikuwa anasumbua tu!jana ndio wakaamua kuachana,binafsi namtakia kila la heri huko aendako
 
Kubaki kwake ingekuwa faraja kwa Yanga lakini Club haiwezi kuwa mateka wa tamaa zake. Aende zake Simba.

Yanga wamefanya la maana sana kutangaza mapema kuwa aende zake. Maana yake ni kwamba Simba nao wanaweza kupunguza dau lao maana hamna tena ushindani wa kumsajili toka Yanga. Atashangaa anaishia kupata hela ndogo kuliko ile ambayo Yanga walikuwa tayari kumpa.

Kila la heri Niyonzima huko matopeni
 
Kwani Ajibu kapewa ngap na Yanga..?
Ukiachana na uwezo wa Haruna..

Bila shaka ana uwezo wenye kupendeza, ila ni bora kuwekeza 70 MILIONI kwa Ajibu kuliko kwa Niyonzima

1. There is still untapped potential kwa Ajibu

2. He's still young ukimlinganisha na Niyo.

3. He's a local ..so it paves a way to recruit foreign player in the club.

4. In terms of final result productivity in midfield area, they equals in terms of goal capability.

5. At least Ajibu can take Free Kicks

Kama Ajibu atahusika msimu ujao, bado silioni pengo la Niyo.
 
Kwa miaka ya karibuni, siku Lunyamila alipoihama Yanga nilijua ndio mwisho wa Yanga...

Lakini haikuwa hivyo, nadhani hata kuondoka kwa fundi huyu hakutaiyumbisha timu.

Niyo kama mchezaji kashafanikiwa kwa karibu kila kitu Yanga, hakukuwa na challenges mpya zaidi ya makombe ya kimataifa ya CAF (ambayo of course hata akienda Simba hatapata)...

Hivyo kwake huu ndio muda wa kupiga mpunga wakati umri na kiwango vinaruhusu...
 
Yaaani naukubali sana uongozi wa Yanga Sc, huwa hawana papara wala mihemko ya ajabu ajabu.

Wanaongoza club kisayansi zaidi (katika sauti ya Mwl kashasha)

3 times undisputed champion
Wachezaji ni wajanja sana. Niyo anaijua vyema tension ya suala la usajili lilivyo akaona ni opportunity ya kujenga fedha....

Sikutarajia kuona angeweka mbele uzalendo na klabu. Hili ndio jambo nililokuwa napenda wachezaji wafanye, uzalendo unawakosesha sana pesa.

Ni kheri kufuata penye pesa zaidi.
 
Ukiachana na uwezo wa Haruna..

Bila shaka ana uwezo wenye kupendeza, ila ni bora kuwekeza 70 MILIONI kwa Ajibu kuliko kwa Niyonzima

1. There is still untapped potential kwa Ajibu

2. He's still young ukimlinganisha na Niyo.

3. He's a local ..so it paves a way to recruit foreign player in the club.

4. In terms of final result productivity in midfield area, they equals in terms of goal capability.

Kama Ajibu atahusika msimu ujao, bado silioni pengo la Niyo.

Sasa itakuwa zamu yao kumsubiri arudi kila akienda kwao.

Alikuwa mchezaji mzuri lakini value ya mchezaji inaendana na umri wake. Je kocha wa Simba atamkubali?
 
Kwa miaka ya karibuni, siku Lunyamila alipoihama Yanga nilijua ndio mwisho wa Yanga...

Lakini haikuwa hivyo, nadhani hata kuondoka kwa fundi huyu hakutaiyumbisha timu.

Niyo kama mchezaji kashafanikiwa kwa karibu kila kitu Yanga, hakukuwa na challenges mpya zaidi ya makombe ya kimataifa ya CAF (ambayo of course hata akienda Simba hatapata)...

Hivyo kwake huu ndio muda wa kupiga mpunga wakati umri na kiwango vinaruhusu...

Hapa nimekuelewa!
 
Sasa itakuwa zamu yao kumsubiri arudi kila akienda kwao.

Alikuwa mchezaji mzuri lakini value ya mchezaji inaendana na umri wake. Je kocha wa Simba atamkubali?

Narudia tena! Licha ya Ubora wake Kwenye Discipline nampa 55%...

Kawaulize wanyarwanda vyema, wanamjua.
 
Hayuko kwenye mipango ya mwalimu ..mechi za kimataifa anacheza chini ya kiwango..anashine mechi za jk ruvu.majimaji nk
Haruna ni aina hiyo ya mchezaji ambaye suala la Ku turn up kwenye big games ....sanasana vs Simba amekuwa si wakutegemewa sana.

Usizungumzie huko kimataifa, performance yake hailingani na perfomance ya mchezaji wa nje inayotegemewa.....

He never impressed me on CAF levels
 
Back
Top Bottom