Fundisho kubwa Sana kwa WCB

Wako wapi wakina juma nature bwana eeee, wote waliojitenga wamepotea mazima.
 
na Diamond alikuwa anajua
 
Hivi kwanini suala la msanii kufika mbali mnalihusisha sana na kuhama label?! Kwanini suala la msanii kukua mnalihusisha na kuhama label?!

Guys, record label is just a business, na ndio maana hakuna msanii duniani anayeitwa Sony Music Entertainment, Colombia Records, Universal, and the like! Kukua na kufika mbali kwa msanii kunategemea na label husika kuifahamu vema biashara ya muziki!! Music Label sio talent house, kwamba pale unaenda kukuza kipaji na baada ya hapo unaenda kujitegemea!!! Mgtu uhami label eti kisa umekua, bali unahama label ikiwa unaona unaokenda kuna maslahi zaidi na kuna uwezekano mkubwa wa kuendeleza career yako!!!

Aidha, Msanii hufiki mbali eti kwa sababu una label yako mwenyewe, bali msanii unafika mbali ikiwa una management mzuri bila kujali label ni yako au hapana!! Leo hii Harmonize akianzisha label yake haita-gurantee ukuaji wake zaidi ya alipo sasa; sana sana, label ikifanya vizuri ita-guarantee tu mapato na sio kukua kimuziki! Lakini ukishindwa kujipanga, sio tu haita-guarantee ukuaji wako bali pia haiwezi ku-guarantee kipato chako, na ndio maana sio kila mwenye label yupo kama mwenzake!

Harmonize angekuwa mjanja asingetoka WCB moja kwa moja bali angeangalia uwezekano wa kubadili mkataba wake kutoka kuwa msanii wa WCB na kuingia publishing contract! Kwamba, kazi zake zote anazifanya kwenye studio yake lakini publishing rights anawapa WCB na hivyo kuendelea ku-capitalize influence ya WCB! Kwenye hiyo studio yake au label, angeweza kusaini hata wasanii wengine ambao nao akatoa publishing rights kwa WCB; kwa sababu, mtake msitake, pale WCB kuna watu wanaoifahamu vema music industry!!!

Narudia, kuwa na label yako mwenyewe hakumfanyi msanii awe mkubwa. kwa sababu mafanikio ya label sio tu suala la wewe kuweza kuingia studio muda wowote na kutengeneza maelefu ya track na bila wa kukuzuia wakati gani utoe ngoma ipi bali it's all about ni namna gani unaifahamu vema biashara ya muziki na tasnia kwa ujumla!! Kinyume cha hayo, utaishia kutengeneza tracks kali lakini sio hit tracks!! Na hapa tukumbushane kwamba, sio kila hit track ni kali; na wala sio kwamba tracks ambazo hazi-hit sio kali!! Mtu kama Diamond anaweza kutoa track ya hovyo kabisa na ika-hit huku Bel 9 akatoa bonge la ngoma, akaishia kusikiliza na washikaji zake hata baada ya kui-release!!

Aidha, tukumbushane kwamba, kuna wasanii kibao tu wenye uwezo kuliko Harmonize na wala hawapo chini ya label ya mtu! Ingekuwa kuwa na label yako ni kutusua, basi tungewaona wao wakitusua kwanza!! Hata Kings Music haijamfanya Ali Kiba kuwa mkubwa kuliko alivyokuwa kabla ya Kings Music!
 
Naunga mkono hoja
 
Hamorapa akachukue namba WCB
Harmonize afanye yote ila hawa watu asiwakwepe hata kidogo
Tale
Fella
 
Reactions: rr4
Amefanya sahihi, kila mtu ana maono tofauti, muda wa kukaa WCB umetosha.. Ili tupate gemu nyingine kwa viwango vingine.. Tatizo la watanzania ni woga wa kudumu. Bora Harmo, ameonyesha njia... Utasikikia kila siku humu, mtu akitaka kujitegemea kwa kuacha kazi anapewa support. Basi na Harmo apewe support hiyo... Nenda Harpo, Maono mapya, Maisha mapya.
 
Umesema vema sana Mkuu, ushauri murua sana kwenye biashara ya muziki. I hope watapita hapa kusoma.
 
Kwa mwaka huu tu Harmonize katoa EP yake ya AFRO BONGO yenye ngoma 4 tena ndani yake amewashirikisha wasanii wakubwa Burna boy, Mr Eiz, Yemi alade na Platnumz, pia akatoa Never give up, katoa Remix na qchilla #myboo na zingine nilizo zisahau

Rayvanny katoa Tetema, na Girlfriend tu

Then unakuja kusema anabaniwa kutoa nyimbo SERIOUSLY?? Yaan wewe ndiyo waku valia njuga kwamba jamaa aondoke WCB wakati hata ABC yake huijui

Ayseeee!! Na Kama type ya mashabiki wake ni Kama wewe Nampa mwaka mmoja tu kwenye game
 

Ongezea hapo mkuu Boss wake Diamond tangia jana mpaka mwaka huu mwezi wa 8 Katoa nyimbo 3 tuu, KANYAGA, INAMA na THE ONE.

Harmonize mwaka jana katoa nyimbo kama 5 hivi achilia hizo za mwaka huu.
 
Nadhani ni bora hata Rayvan anaweza kulalamika maana yeye collabo zake ni Diamond tu,chache sana za wasanii wakubwa wa nje kuliko Harmonize.
TRUE! Mtu wala ahitaji macho matatu kuona kati ya wasanii WOTE walisainiwa WCB, ni Harmonize ndie alikuwa anapendelewa zaidi hasa linapokuja suala la utoaji ngoma na collabo! Tena nadhani, ukihesabu kuanzia pale alipoingia, unaweza kukuta yeye ndie katoa ngoma nyingi zaidi pengine kuzidi hata Diamond; halafu anakuja mtu anadai eti alikuwa anabaniwa!!!
 
Rayvanny naye ajipange kusimama mwenyewe la sivyo atakuja kubwagiwa mabegi umuhimu wake wa kuwatungia mashairi utapoisha!
 
Harmonize Ana kipaji na kilihitaji skilled manager ili afike mbali. Pele limepata mkunaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…