Funga au Ondoa Programu Tumizi (App) usizotumia au zilizopitwa na wakati ili kuimarisha usalama na kulinda taarifa zako Mitandaoni

Funga au Ondoa Programu Tumizi (App) usizotumia au zilizopitwa na wakati ili kuimarisha usalama na kulinda taarifa zako Mitandaoni

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Jinsi ya kufuta Programu Usizotumia au zilizopitwa na wakati

1. Programu Endeshi Android:
Fungua Google Play Store > Upande wa Juu Kulia, Bofya alama ya ‘Profile’ > Kisha Bofya ‘Manage App & Devices > Bofya ‘Manage’ > Changua ‘App’ unayotaka kuondoa > Bofya ‘Unistall’

2. Programu Endeshi - iOS
Bofya Mipangilio (Settings) > Kisha 'General' > Halafu 'iPhone Storage' > Chagua 'App' unayotaka kuiondoa > Bofya 'Offload App' ikiwa unataka ikupe nafasi ila taarifa zake zibaki AU bofya 'Delete App' ikiwa unataka kuiondoa na taarifa zake
Ni muhimu kufuta au kufunga programu ambazo huzitumii au zilizopitwa na wakati kwani vinaweza kuendelea kukusanya taarifa zako

Aidha, Programu ambazo hazijatumika kwa muda mrefu zina hatari kubwa zaidi ya kushambuliwa na wadukuzi au kuvujisha taarifa binafsi.

Pia, kifaa chako kitaenda kwa kasi zaidi endapo programu na faili zisizotumika zitafutwa.
 
Back
Top Bottom