Fungu la elimu ya Juu Zanzibar

Fungu la elimu ya Juu Zanzibar

Vikosi vya SMZ,KMKM Huwa unalipa wewe?

Swali; Kuna Mzanzibari aliwahi kuja Bara akasema anahitaji Muungano?

Wewe Kwa akili Yako hujiulizi Kwa nini Bara wanalazimisha Muungano? Jibu ni wanafaidika kuliko wanachotoa ,by the way hawatoi pesa zote zinatoka Zanzibar.

Kama mna jeuri , vunjeni Muungano tuone au umesikia Wazanzibar wanataka Muungano? 🤣🤣🤣🤣

Hata Rais wa Zenj mnawazuga yule Mwinyi ni Mtanganyika.

Badala ya kulia lia kama mtoto ni Bora Waendelee kuongeza hizo GBS Hadi mkome,si mlitaka Muungano ndio Raha na gharama zake hizo.
🤣 🤣 🤣 👊
 
Tatizo unakimbilia kujibu kabla ya kusoma na kuelewa. TRA Zanzibar, inakusanya kodi Zanzibar lakini pesa inayokusanywa haipelekwi kwenye kapu la Muungano badala yake inatumika yote huko huko kugharamia mambo ambayo ni ya Muungano Zanzibar. Na huwa haitoshi, hivyo Tanganyika kulazimika kupeleka pesa nyingine Zanzibar iliyokusantwa Tanganyika.
🙋‍♂️✍️👊👍👏
 
1. Wazanzibar kwenye masuala ya elimu, kule kwao wana fungu la Elimu ya Juu Kwa watu wa Zanzibar na sio mkopo , Lakini Hii mikopo yetu huku HESLB kuna kifungu tena cha Wazanzibar, yaani hiyo fedha ni kwa ajili ya Wazanzibar tu, Yaani fedha ya Tanganyika inatumika HESLB ambayo imekusanywa na TRA huku Tanganyika inakwenda Zanzibar kuhudumia mikopo ya Elimu ya juu
Halafu wao walishakataa siyo watanzania ni masalia ya Sultan, pamoja na mama yao
 
Hapo hapo anatokea mzanzibar anasema Tanganyika wanainyonya Zanzibar,,,muungano wa kidwanzi kuwahi kutokea
 
Chawa Kwa sasa TRA zanzibar haina makusanyo zaidi ya bilioni 2 , ZRA imechukua kila eneo la TRA na watumishi wa TRA kule wanalia kila siku, hakuna tena TRA kule imebaki story tu, endelea kupiga makofi sasa
Wewe nyumbu hii ni nini hapa ? 👇👇
Screenshot_20240611-091742.jpg
Screenshot_20240611-091717.jpg
Screenshot_20240611-091628.jpg
 
Wazanzibari hawaelewi. Wanadanganywa na wajinga wenzao kuwa eti bila Muungano wangekuwa vizuri sana, lakini ukweli ni kuwa Zanzibar leo hii ikiwa nje ya Muungano, itakywa maskini kuliko hata Burundi. Zanzibar na Wazanzibari wanatunzwa na Tanganyika.

Wajaribu watoke kwenye Muungano waone watakavyokuwa.
Acha kuongea stori za kufikirika wewe nyumbu.Huo umaskini utokee wapi wakati Wana Rasilimali na wako wachache?

Pili Zenj ukiacha Utalii Wana Mafuta,karafuu na uvuvi wa bahari.

Kama Mauritius imeendelea na Haina chochote sembuse Zanzibar?
 
The sunk,

Mtoa mada amedai kwamba Znz inachukua mkopo na Tanganyika ndio huwa na jukumu la kulipa akatolea mfano wa mkopo sac korea wa kujengea hospitali.

Na pia amezungumzia kuhusu Mama samia kubadilisha 4.5% mpaka 9% na si mkopo tunawapa kwa madai ya mtoa hoja. Sasa TRA Kwanini wawe wanawakandamiza Auckland Tanganyika iwe inawakandamiza watu 1.5 milioni kwa mlinganyo wa watu 60milioni?

Mkuu the sunk,

Vipi kuhusu wabunge ambao wapo huku pesa za kuwalipa na gharama huwa zinatoka wapi?

Lakini pia mtoa mada amesema kwa sasa Znz ina TRA yao na wanakusanya mapato yao na wanatumia huko huko sasa anadai Kwanini tutoe pesa ya kuhudumia Elimu ya juu ya kwao?

Mtoa mada ni mpotoshaji,

Kuna mikopo ya aina mbili, Mikopo inayokopwa na JMT na mikopo inayokopwa na SMZ huku SMT ikiwa kama Dhamana.
Mikopo ya SMZ inalipwa na SMZ wenyewe, na ndio mana kama umetizama mikituno ya Jussa karibuni amekuwa akiishamublia sana serikali ya Dr Mwinyi kuhusu mikipo kuwa mengi kupindukia.

Mikopo ya SMT ni mikopo ya Muungano, Zanzibar hupata gawio lake la mikopo hiyo pale inapokopwa, Hii mikopo hulipwa na SMT kwa kupitia source za mapato za Muungano.
 
Hiyo ya Zanzibar kupewa 9% badala ya 4.5% ni hakika labda kama umebweteka hufuatilii taarifa mbalimbali.

Taarifa iliwekwa wazi, hata kwenye ule mkopo wa Covid 19 ilielezwa wazi kwa kuzingatia hivyo vigezo vipya vya Samia.
Wanasoma basi? Wao wanasubiri kusikiliza OMO na Jussa wamesema nini!
 
.

Mikopo ya SMT ni mikopo ya Muungano, Zanzibar hupata gawio lake la mikopo hiyo pale inapokopwa, Hii mikopo hulipwa na SMT kwa kupitia source za mapato za Muungano.
Tueleze source za mapato ni zipi?
 
Mtoa mada ni mpotoshaji,

Kuna mikopo ya aina mbili, Mikopo inayokopwa na JMT na mikopo inayokopwa na SMZ huku SMT ikiwa kama Dhamana.
Mikopo ya SMZ inalipwa na SMZ wenyewe, na ndio mana kama umetizama mikituno ya Jussa karibuni amekuwa akiishamublia sana serikali ya Dr Mwinyi kuhusu mikipo kuwa mengi kupindukia.

Mikopo ya SMT ni mikopo ya Muungano, Zanzibar hupata gawio lake la mikopo hiyo pale inapokopwa, Hii mikopo hulipwa na SMT kwa kupitia source za mapato za Muungano.
source zipi? fafanue, ile gawio la mkopo tunaokopa wao huwa wanalipaje ile asilimia yao waliyopewa. tutalea hadi lini hawa watu? tunafaidika nini nao?
 
Bara imeenda Zanzibar kufanya nini?
Jaribu kuwa mfuatiliaji kidogo mkuu
1. Kipindi cha Ijue Benji kuu kinarushwa na TBC1. Kule ndani kuna afisa wizara ya fedha Zanzibar anaishukuru BOT kulipa mishahara Zanzibar kipindi cha Covid 2019.

2. Kipindi cha Bunge la Katiba Rasimu ya Warioba ilikuwa na serikali 3. Fuatilia mchango wa waziri kiongozi mstaafu Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha alikataa katakata kuhusu serikali 3 na kutaka zibaki 2 kama ilivyo huku akitaja faida lukuki Wazanzibari wanazozipata ndani ya muungano. Moja wapo alisema kuna wazanzibari wanamiliki mashamba makubwa ambapo hata huko Zanzibar wasingeweza kupata ardhi ya ukubwa huo. Alisema ZNZ ni kisiwa hakiongezeki na idadi ya watu inaongezeka hivyo baada ya muda hata sehemu ya kuchimba mchanga itakosekana.
 
source zipi? fafanue, ile gawio la mkopo tunaokopa wao huwa wanalipaje ile asilimia yao waliyopewa. tutalea hadi lini hawa watu? tunafaidika nini nao?

asilimia wanayopewa hulipwa na mapato ya JMT, sasa kigumu ni kipi kuelewa mkuu?
 
mapato yepi ambayo sisi tunashea kuyapata na zenji?

Kodi yoyote inayokusanywa na TRA (ukiotoa VAT)
kama income Tax za makampuni na biashara, Paye, Ushuru wa Forodha
Tozo za aina zote e.g za mitandao ya simu
Visa fees
leseni zote za mashirka kuanzia, makampuni ya simu, ma bank
Mapato ya Anga
Misaada
fain zote zinazotokana na Wizara za Muungano

Hayo kwa uchache tu
 
Tuna maviongozi ya hovyo sana hapa Tanganyika sijawahi kuona,majitu yamesoma lkn bado majinga,hayaoni Tanganyika inavyopelekeshwa na nchi ndogo ya watu m2 yaani Zanzibar
 
Kodi yoyote inayokusanywa na TRA (ukiotoa VAT)
kama income Tax za makampuni na biashara, Paye, Ushuru wa Forodha
Tozo za aina zote e.g za mitandao ya simu
Visa fees
leseni zote za mashirka kuanzia, makampuni ya simu, ma bank
Mapato ya Anga
Misaada
fain zote zinazotokana na Wizara za Muungano

Hayo kwa uchache tu
haya yote umeyataja, ni makusanyo ya mapato Tanganyika, kwasababu zanzibar wana ZRA yao. kama mitandao wanayo ya kwao zantel. swali letu lilikua ni, kwasababu zanzibar wana ukusanyaji kodi wa binafsi ukitofautisha ule wa bara, kwanini makusanyo ya bara yalipe deni ilikudingi asilimia alizokula zenji?
 
Back
Top Bottom