Fungua Milango ya Mafanikio: hizi ndizo njia kwa wanaume kujiondoa katika umaskini

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Pata Mwanamke Sahihi

1736858532635.png

Sahau kuhusu slay queens na wanawake wenye sura na shape wasioweza kukuunga maono yako. Tafuta mwanamke atakayekuunga mkono kwenye maono yako na kukupa ahueni kwenye safari ya kusaka mafanikio. Mwanamke alie tayari kutimiza majukumu yake na yenu kwa pamoja, ni muhimu sana kumtesti kama anajiongeza kufanya majukumu yake kabla ya ndoa kama kupika chakula, usafi wa ndani, kudeki, n.k. Usijichanganye kuoa girlfriend anaeshinda kwenye mitandao, kutwa nzima kupiga soga na mashosti, shughuli hazimpiti, anapenda kuagiza kyepe yai badala ya kupika, hana nidhamu ya fedha yeye anawaza matumizi bila kuheshimu jasho la kuipata pesa, n.k.

Acha Uvivu

1736858603436.png

“Ee Mwanamume, kwa nini umekuwa mvivu?” Wewe ni mvivu kupindukia. Unapenda kulala, kushinda mitandaoni, kucheza game, kuvuta bangi / kunywa pombe bila kazi na kushinda vijiweni na kulaumu serikali kwa umaskini wako. Wanaume wengi wavivu wana nguvu ya kwenda raundi tatu mpaka tano kwa mwanamke lakini hawana nguvu hata ya kutengeneza vibanio vya kuanikia nguo waviuze,

Fuatilia Mambo ya kukuletea maendeleo - Ukiweka takataka nyingi kichwani, maisha yako yatakuwa takataka. kuna wanaume wapo active sana kwenye mada za ngono, soka, siasa, nani ni tajiri na nani si tajiri, nani ana nyumba nzuri, Lakini ukileta mada za uwekezaji, ubunifu, au biashara, wanashika simu zao, wanapiga miayo, au kuaga ghafla. Mwanaume masikini lazima ujikite kuendelea kujifunza chochote cha kukuletea maendeleo, Hata kama una degree kama huna kazi jifunze ujuzi wowote unaoweza kukuletea maendeleo

1736858804738.png

Jichanganye na watu waliokuzidi - Sisemi uvunje urafiki na uliowazidi au kulindana, No ! Wanaume wengi wanashindwa kwa sababu hawana mentors wa kuwaonyesha njia. Hawana mtu wa kukaa naye chini wa kuwapa madini. Zamani, wazee walikaa na vijana wakawafundisha jinsi ya kuwinda na kuua wanyama na hakuna kijana aliyekuwa mwanaume kamili mpaka ameua mnyama mwenyewe ili aweze kuanza kujitegemea na kuanzisha familia. Ukienda sehemu za mijumuiko mfano bar / pub za bei chee jua unajihusisha na watu wenye uwezo mdogo kimaisha na wenye ideas, connections na motivations ndogo, Wanakushangilia ukiingia mkubwa wao umefika. Sometimes nenda bar au sehemu za mijumuiko high class, huko unaweza kupata connections, ideas na mentors waliokuzidi wakakupa ramani.

1736858879213.png

Punguza kutegemea miujiza / Ndumba / Kusali sana - Acha kutumia siku nzima kuomba na kufunga huku unajua Quran na Biblia zote zinasema Mungu hubariki kazi za mikono yako. baraka zinakupata ukiwa njiani ukifanya jambo. Acha kutumia maombi kama kisingizio cha kutojishughulisha. Fanya kazi kwa bidii. Ni kosa mifuko yako kuwa mitupu na kichwa chako pia kuwa kitupu.

1736858986385.png

Darasa Limefungwa.
 
  • Pata Mwanamke Sahihi - Sahau kuhusu slay queens na wanawake wa sura lakini hawana akili. Tafuta mwanamke atakayekuunga mkono kwenye maono yako na kukusukuma kufanikisha zaidi. Mwanamke atakayekutengenezea mazingira ufanye shughuli zako kwa bidii huku nae akiwa msaada kwa namna moja au nyingine, sio mwanamke anaeshinda kwenye mitandao, kutwa nzima kupiga soga na mashosti, shughuli hazimpiti, hana nidhamu ya fedha, n.k.
  • Acha Uvivu - “Ee Mwanamume, kwa nini umekuwa mvivu?” Wewe ni mvivu kupindukia. Unapenda kulala, kushinda mitandaoni na kushinda vijiweni na kulaumu serikali kwa umaskini wako. Wanaume wengi wavivu wana nguvu ya kwenda raundi tatu mpaka tano kwa mwanamke lakini hawana nguvu hata ya kutengeneza vibanio vya kuanikia nguo waviuze,
  • Fuatilia Mambo ya kukuletea maendeleo - Ukiweka takataka nyingi kichwani, maisha yako yatakuwa takataka. kuna wanaume wapo active sana kwenye mada za ngono, soka, siasa, nani ni tajiri na nani si tajiri, nani ana nyumba nzuri, Lakini ukileta mada za uwekezaji, ubunifu, au biashara, wanashika simu zao, wanapiga miayo, au kuaga ghafla. Mwanaume lazima ajue angalau kitu kimoja cha kumletea maendeleo, Jifunze ujuzi hata kama hujapitia chuo kikuu.
  • Ungana na Watu Wakubwa Kukuzidi - Wanaume wengi wanashindwa kwa sababu hawana mentors wa kuwaonyesha njia. Hawana mtu wa kukaa naye chini wa kuwapa madini. Zamani, wazee walikaa na vijana wakawafundisha jinsi ya kuwinda na kuua wanyama na hakuna kijana aliyekuwa mwanaume kamili mpaka ameua mnyama mwenyewe ili aweze kuanza kujitegemea na kuanzisha familia. Ukienda sehemu za mijumuiko mfano bar / pub za bei chee jua unajihusisha na watu wenye uwezo mdogo kimaisha na wenye ideas, connections na motivations ndogo, Wanakushangilia ukiingia mkubwa wao umefika. Sometimes nenda bar au sehemu za mijumuiko high class, huko unaweza kupata connections, ideas na mentors waliokuzidi wakakupa ramani.
  • Punguza kutegemea miujiza / Ndumba / Kusali sana - Acha kutumia siku nzima kuomba na kufunga huku unajua Quran na Biblia zote zinasema Mungu hubariki kazi za mikono yako. baraka zinakupata ukiwa njiani ukifanya jambo. Acha kutumia maombi kama kisingizio cha kutojishughulisha. Fanya kazi kwa bidii. Ni kosa mifuko yako kuwa mitupu na kichwa chako pia kuwa kitupu.

    Darasa Limefungwa.
Ujumbe kwa atakayeupokea na aupokee ingawaje sio sheria
 
Hahaha kweli
 
Nakumbuka siku moja nimejilipua kwenda Golden Folk Dodoma (chai pekee ilikuwa 5k) nikikutana na Mzee mmoja mwenye busara zake alinipa madini mengi sana. Toka siku hiyo imebidi niwe naenda sehemu zenye hadhi kiasi wakati mwingine nakutana na wageni kutoka Kenya na sehemu zingine inasaidia kuamsha ubongo uliolala.
 
Nahitaji unigawie kidogo hizo almasi mkuu
 
Kivumbi upo kwenye ndoa tayari na una mwanamke mwenye sifa hizo inakuaje?
Binafsi nina bro wangu yule mke wake Mungu amsaidie yaani ni mvivu na mchafu mchafu hadi huruma.
 
Back
Top Bottom