CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Kilichotokea nchini Mali na nchi mbalimbali duniani kuhusu viongozi madikteta kuondolewa madarakani kinatoa somo kwa maafisa waandamizi wa serikali ya Tanzania kwamba kwa kuwa hawaijui kesho yao basi ni vema kutenda haki na usawa kwa watu wote bila kujali vyama vyao vya siasa kwa kufuata katiba na sheria za nchi.
Ni bora kujiuzulu ikiwa agizo la Rais linapingana na katiba na sheria za nchi kuliko kushiriki katika uovu ambao utakuja kuwagharimu siku za usoni siku ambapo mnayemtetea mbele za watu hatokuwa na nguvu ya kuendelea kuwalinda.
Heshimuni vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria kwani leo ni CCM kesho ni CHADEMA. Dunia inakwenda kwa kasi sana na mabadiliko ya upepo wa kisiasa ni suala la siku moja tu.
KWA LEO NI HAYO TU, NAWATAKIA SIKU NJEMA