Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

Funzo la mapinduzi toka nchini Mali: Maafisa waaandamizi wa Serikali ya Tanzania tendeni haki na kwa usawa kwani hamuijui kesho yenu

CreativityCode,
Unapoteza muda tu! Kwa akili yako unaamini Tz iko kundi la nchi kama hiyo Mali? Unaijua Mali au unadandia kila kinachojitokeza? Someni muongeze uelewa badala ya kila siku kuhangaikia whatsapp!
 
Mkuu, huyu ameshindwa kuandika ukweli, kilichomfurumusha huyo Raisi wa Mali ni kushindwa kudhibiti ufisadi ndani ya nchi yake, Jeshi likaona haina Maana kuwa wajeda waendelee kuona wizi ukitamalaki Wakati raia wengi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya mateso na dhiki Ili Hali Utajiri wa nchi Yao ukigawanwa na wachache

Sasa anapokuja kulinganisha na hapa, Kwa kigezo kipi mpaka aseme Eti ni Bora hata hapa kufanyike kama Mali,

Nchi inavyojengwa kiasi hicho, kila mtu anaishi Kwa nguvu zake yeye mwenyewe, na Pesa inayopatikana inaonekana inafanya vitu, mafisadi wamebanwa mbavu hawapumui, Raisi aliyepo Sio pandikizi ni Mtanzania aliyewekwa na Watanzania,

Kwanza hao mapandikizi ndio inabidi wakataliwe kote Africa Ili Africa isonge mbele
Sio ufisadi tu, hali ya uchumi mbaya na pia hali ya usalama wa nchi haiko sawa. Yani kule hawakukubali watu wachache wanatajirika wakati 1.5 trl zinapotea bila maelezo yeyote.
 
Mkuu, huyu ameshindwa kuandika ukweli, kilichomfurumusha huyo Raisi wa Mali ni kushindwa kudhibiti ufisadi ndani ya nchi yake, Jeshi likaona haina Maana kuwa wajeda waendelee kuona wizi ukitamalaki Wakati raia wengi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya mateso na dhiki Ili Hali Utajiri wa nchi Yao ukigawanwa na wachache

Sasa anapokuja kulinganisha na hapa, Kwa kigezo kipi mpaka aseme Eti ni Bora hata hapa kufanyike kama Mali,

Nchi inavyojengwa kiasi hicho, kila mtu anaishi Kwa nguvu zake yeye mwenyewe, na Pesa inayopatikana inaonekana inafanya vitu, mafisadi wamebanwa mbavu hawapumui, Raisi aliyepo Sio pandikizi ni Mtanzania aliyewekwa na Watanzania,

Kwanza hao mapandikizi ndio inabidi wakataliwe kote Africa Ili Africa isonge mbele
Ukiona hivyo, huyu CreativityCode aliyejiunga na JF mwezi August 2020, hajakomaa na huenda kapigwa kibano cha ufisadi na Magufuli na sasa anaamini au anaomba hayo yatokee, akiamini atapata nafuu.
 
Wanajeshi watakachofanya ni kukuheshimu.

Ila ikitikea wananchi wameandamana sana hawakutaki na maandamano yakiwa serious hao wanajeshi wanakugeuka dakika sifuri tu.
Tena wale wa chini, sio wale washakaji wa kuwekana juu.
 
Nani angeamini Mugabe angeondolewa na jeshi? Mpigania uhuru aliyepo madarakani, aliyewatoa kwenye mikono ya wakoloni
Naona umejiunga tangu 2012. Hata kama ulikuwa form 2 sasa hivi ulistahili uwe na uelewa wa kiasi fulani. Unapotoa mfano wa Mugabe na kuondolewa kwake ni ishara tena ya umbumbumbu! Yaani hata Zimbabwe na Mugabe hujui hali ilikuwaje.
 
Wewe unayejua Mkuu haya tuambie sisi mambumbumbu ilikuaje.
 
Jeshi la Mali Jana lilimkamata Rais wa Mali Aboubakar Keita na waziri wake mkuu na kuwalazimisha wajiuzulu Leo asubuhi , hii ni kufuatia maandamano ya nchi ya nguvu za umma kwa miezi isiyopungua mitatu, Rais kajiuzulu kavunja bunge na baraza la mawaziri , kitu cha kushangaza ambacho ni nadra kufanyika katika mapinduzi ni kwamba waliofanya mapinduzi ni Wanajeshi wa vyeo vya chini na wasiokuwa na vyeo kabisa , Wenye madaraka jifunzeni dunia inazunguka hasa Limbukeni wa kihutu ,Belarus nguvu ya umma inaendelea kumwondoa LukashenkoView attachment 1542089
Wamesema aliyeongoza ni kanali wa jeshi, sema tu ni very young...
Screenshot_20200819-153356.jpg
 
Sio ufisadi tu, hali ya uchumi mbaya na pia hali ya usalama wa nchi haiko sawa. Yani kule hawakukubali watu wachache wanatajirika walati 1.5 trl zinapotea bila maelezo yeyote
Mkuu, nadhani hapa kwetu iko shida ya Idara moja hivi kutokuwekwa mambo yake peupe pe
 
CreativityCode,

Ndugu yangu ogopa sana maofisa wa Jeshi wenye vyuo vya Luteni Usu, Luteni, Captain, Meja, Luteni kanali na Kanali . Hawa watu ni watu wenye ujasiri sana na uwezo mkubwa sana.

Nyerere angekuwa hai angekueleza maofisa wa vyeo hivi walivyomwendesha!

Hao kina Luteni Maganga, Captain Kadego na Meja Khatib Macghee bado kidogo wamuondoe Baba Makongoro magogoni mwaka 1982
 
Unapoteza muda tu! Kwa akili yako unaamini Tz iko kundi la nchi kama hiyo Mali? Unaijua Mali au unadandia kila kinachojitokeza? Someni muongeze uelewa badala ya kila siku kuhangaikia whatsapp!
Sidhani kama Mali waliwahi fika hatua ya kuteka na kuua watu na kumiminia watu risasi 38 mchana wa saa saba.

Unaweza ukawa unanufaika na regime hii, wenye familia za wahanga wanajua jinsi gani ya kuifafanua TZ.

Kama ww uko safe na hujaguswa piga kimya.
 
Ukiona hivyo, huyu CreativityCode aliyejiunga na JF mwezi August 2020, hajakomaa na huenda kapigwa kibano cha ufisadi na Magufuli na sasa anaamini au anaomba hayo yatokee, akiamini atapata nafuu.
Ni upumbavu wa kiwango cha juu sana kufikiri kila anayepinga uovu wa serikali ya awamu ya tano ama katumwa na mabeberu au alikuwa fisadi na sasa mirija yake imezibwa.

Ni usukule wa kiwango cha kutisha na kuogofya kuona kwamba awamu hii inaongozwa na "malaika".
 
If the government refuse to develop the region

And continue the marginalization and injustice

The youth, that’s what coming after us

And it will be more brutal than what we have done.
 
Wewe unayejua Mkuu haya tuambie sisi mambumbumbu ilikuaje.
Niulize unachotaka kujua. Uchumi wa Zimbabwe? Nguvu ya Mugabe Jeshini (Comrades), afya yake? Uwe specific maana nionavyo wote tuko JF kama bahari. Kuna uduvi hadi nyangumi.
 
Back
Top Bottom