Viongozi mbalimbali wa Chadema wametupa uwazi na kioo cha kuangalia jamii yetu ya Tanzania ilivyo, ilipo na inapokwenda. Chadema tumeona viongozi wasomi, wavumilivu, watukutu, wabishi, wasiojielewa, majasiri, masikini na matajiri. Hii yote imekuwa kama sampuli ambayo ipo kwenye wanasiasa wetu wote bila kujali chama.
1. Kuna Kundi ambalo lina watu wanajielewa na wamejitosheleza. Hawa sio wasomi tu ni mchanganyiko. Hili ni kundi ambalo ni ngumu kuwanunua kwa pesa kwasababu imani zao sio kwao ni kwa vizazi vijavyo hawa ni kama Lema, Sugu na Mbowe na wengine wengi ambao siwajui. Hawa wote kwa maneno yao wamesema walishapewa pesa na ahadi za vyeo wahame lakini walikataa na mimi naamini hili. Hawa wanaamini kwenye demokrasia lakini zaidi hawa wanaamini kwenye mafanikio binafsi ya watu au mfumo wa capitalist. Lema ambaye anajiita hasla amaamini anaweza kufanikiwa sehemu yeyote ili Duniani ilimradi awe na usalama na haki. Hii inami ipo kwa hawa wote.
2. Kundi ambalo lingine ni wale ambao ni wasomi lakini sio wafanyabiashara mfano Lissu na Msigwa. Lissu anaamini wananchi zaidi kuliko pesa tofauti na kikundi cha kwanza. Lissu na msigwa ana amini ni muhimu kuweza kujikimu lakini sio lazima uwe tajiri tofauti na group ile ya pale juu. Naamini hili group pia haliongeki lakini akitokea mtu ndani ya CCM amabye wanamwamini na wakamwambia tunaomba uje tubailishe nchi pamoja na kubadilisha katiba pamoja wanaenda mfano mzuri ni Raisi wa Zanzibar. Raisi Mwinyi angekuwa Raisi wa Tanzania na awe na nia njema hawa wangeweza kuondoka maana wanajali zaidi nchi kuliko watu.
3. Wasomi njaa: Hawa ni wale wasomi wa Chadema wenye kuamini makundi ya hapo juu lakini hawana mbinu za kujiendeleza kiuchumi na hivyo kulazimika kutegemea serikali kwa maslahi yao. Pamoja na kukubaliana na Chadema na viongozi wake wanaangalia chakula chao kwanza ili waweze kuwa na maisha mazuri. Hawa ni wakina Mdee, Dr Mollel, Mkumbo, Dr Slaa na Zitto. wote hawa wana nia nzuri lakini hawana uwezo. Hawa ni wale ambao wana nunulika na kujiaminisha tutabalisha nchi mbele kwa mbele
4. Kundi la lingine ni wale walioingia Chadema lakin i wakiwa njiani kwenda CCM. Kuna wanasiasa kama Nyalandu, Lowassa ba Member ambao kuingia na kutoaka Chadema walifikiri kutawapandisha chat lakini mpaka sasa haikuwa hivyo
5. Kuna kundi la mwisho ambalo wenyewe kutokana na majanga waliopata, hali ya maisha na rushwa watakuwa wapinzani tu bila kujali hoja wala nini ilimradi CCM iko madarakani wenyewe watakuwa wapinzani.
Kwa mawazo yangu tunahitaji wapinzani ambao hawa nunuliki, wanajitegemea kiuchumi, hawana visasi na wanaweza kubalika. Tanzania inashangaza wasomi hata miradi ya kuku hawawezi kuendeleza? hii inasababisha tuwe na watu kama Bushiru ambao wanaongea kwa pande mbili za midomo.