Hayupo Rais mwingine atakayekuja kutawala nchi hii halafu akafanyiwa hujuma kama alizofanyiwa hayati JPM
Kwa machache tu, mara baada tu ya kuingia madarakani
MOJA: Lundo la wanafunzi wakafukuzwa kule UDOM, akiambiwa kuwa walikuwa wanasoma degree wakiwa hawana qualifications. Possibly kweli baadhi yao hawakuwa na qualifications ila NAMNA ile ya kuwaondoa watu hao ndiyo HUJUMA zilipitishiwa humo. Waliondolewa kwa utaribu utafikiri ni wahalifu wa kiwango cha juu kabisa, wakati walikuwa ni wa-Tanazania wazalendo na watoto wa wakulima. Sisemi kwamba kuondolewa wanafunzi hawa haikuwa sahihi, bali NAMNA walivyoondolewa nsdiyo haikuwa sahihi
MBILI: Wafanyakazi hewa na wale ambao hawakuwa na elimu stahiki. Hapa walikuwa wanaingizwa na wafanyakazi wengine ambao hawakustahili kuwemo kwenye makundi hayo
TATU: SUKUMA GANG- Hili kundi linaweza kuwa kweli lilikuwepo, lakini ukweli ni kuwa kama kweli lilikuwa ni la WASUKUMA, basi lilikuwa limeundwa kwa ajjili ya kumchafua, na siri hiyo ilikuwa inajulikana na WASUKUMA wachache wale waliokuwa wameasisi kundi hilo, na possibly waasisi wa kundi hilo hawakuwa WASUKUMA na ndiyo maana ilitumika njia ya kusambaza kwanza CLIP ya msukuma waliyemsingizia kuwa ana mpango wa kuanzisha kundi la ina hiyo.
Chances kubwa ni kwamba waasisi wa kundi hili wanaweza kuwa hawakuwa WASUKUMA
NNE: Mh. Tundu Lissu kujeruhiwa kwa mvua za risasi. Ni kundi hilo hilo la kumhujumu Magufuli lilikuwa liko kazini
Mambo ni mengi ikiwa ni pamoja na ya kule KIBITI pamoja na matukio ya kwenye mto Ruvu
"USIPOMPENDA RAIS ALIYEKO MADARAKANI, IPENDE NCHI YAKO"