Furaha Dominic leo ataendelea na Mahojiano. Je, atawataja Kupe waliomnyonya hayati Magufuli?

Huu ni umbeya tuu. Hivi muandaaji wa kipindi unamuandaaje mtu mmoja kushambulia bila mtuhumiwa kujibu?
Binafsi namchukia Gwajima lakini mahojiano ya juzi hayakuwa sahihi. Nitashangaa na leo akaendelea nayo
 
Hawezi kuwataja hapo ndo amefikia mwisho. Anatafuta huruma ya kukumbukwa kwenye teuzi ama anajipanga kwa ajili ya 2025.
Hajifunzi kwa Marehemu dada yetu Amina Chifupa. Kutishia kutaja ni kujitundika kitanzini, ni ama wawai kukata kitanzi vinginevyo unaondoka.
====
Kwa nini hakumueleza KUPE hao Hayati Dr J. Magufuli?
 
Hayupo Rais mwingine atakayekuja kutawala nchi hii halafu akafanyiwa hujuma kama alizofanyiwa hayati JPM
Kwa machache tu, mara baada tu ya kuingia madarakani
MOJA: Lundo la wanafunzi wakafukuzwa kule UDOM, akiambiwa kuwa walikuwa wanasoma degree wakiwa hawana qualifications. Possibly kweli baadhi yao hawakuwa na qualifications ila NAMNA ile ya kuwaondoa watu hao ndiyo HUJUMA zilipitishiwa humo. Waliondolewa kwa utaribu utafikiri ni wahalifu wa kiwango cha juu kabisa, wakati walikuwa ni wa-Tanazania wazalendo na watoto wa wakulima. Sisemi kwamba kuondolewa wanafunzi hawa haikuwa sahihi, bali NAMNA walivyoondolewa nsdiyo haikuwa sahihi

MBILI: Wafanyakazi hewa na wale ambao hawakuwa na elimu stahiki. Hapa walikuwa wanaingizwa na wafanyakazi wengine ambao hawakustahili kuwemo kwenye makundi hayo

TATU: SUKUMA GANG- Hili kundi linaweza kuwa kweli lilikuwepo, lakini ukweli ni kuwa kama kweli lilikuwa ni la WASUKUMA, basi lilikuwa limeundwa kwa ajjili ya kumchafua, na siri hiyo ilikuwa inajulikana na WASUKUMA wachache wale waliokuwa wameasisi kundi hilo, na possibly waasisi wa kundi hilo hawakuwa WASUKUMA na ndiyo maana ilitumika njia ya kusambaza kwanza CLIP ya msukuma waliyemsingizia kuwa ana mpango wa kuanzisha kundi la ina hiyo.
Chances kubwa ni kwamba waasisi wa kundi hili wanaweza kuwa hawakuwa WASUKUMA

NNE: Mh. Tundu Lissu kujeruhiwa kwa mvua za risasi. Ni kundi hilo hilo la kumhujumu Magufuli lilikuwa liko kazini

Mambo ni mengi ikiwa ni pamoja na ya kule KIBITI pamoja na matukio ya kwenye mto Ruvu

"USIPOMPENDA RAIS ALIYEKO MADARAKANI, IPENDE NCHI YAKO"
 
Ni Vema AKAWATAJA MAANA MAGUFULI ANALAUMIWA KILA KITU NA MASWAHIBA WAKE

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Acha utopolo wa kumtetea rais katili kuliko yeyote kutokea Tanzania.
Kwa Ben Saanane anasingiziwa?
Kwa Lissu, aliwahi saidia lolote, na atasaidia vipi kama alihusika!
Uteuzi wa mawaziri predominantly toka Geita na kanda ya Ziwa, alikuwa amefumba macho?
Kuuwawa Lwajabe, na maelezo yasiyoeleweka, alihusika vipi?
Wizi wa Trillioni 1.5, na kufukuzwa CAG aliyelaumu wizi huo, anahusika vipi?

Mambo ni mengi yaliyowazi, yaliyojificha yatajulikana tu.
 
Kwa Lissu aliwahi saidia lolote, na atasaidia vipi kama alihusika!
Unatia moyo kwa sababu angalau inaonyesha unaziona mwenywewe hujuma nyingine alizokuwa anafanyiwa. Mimi sisemi kwamba aikuwa ni malaika, isipokuwa najaribu tu kuaanisha yale ambayo yalifanywa kwa nia ya kumhujumu.

In fact mtu hawezi kumhujumu Rais aliyeko madarakani, except anaweza kuihujumu nchi na si vinginevyo
 
No.2 uko sahihi, kuna wengine wamerudishwa kazini baada ya miaka 3. Kuna mmoja aliondolewa kazini kisa tu alipoajiriwa toka kwao Bukene ndani huko hakuwa na dini, baada ya miaka 3 akaokoka na kubatizwa. Akaapa Mahakamani jina la Joseph likongezwa kwenye majina yake. Kumbuka cheti cha form 4 cha 1981 kina majina 2 tu. Eti hilo likawa kosa la kuonesha ni mtumishi hewa??
Kuhusu LISSU yawezekana uko sahihi kwamba hakujua mpango mzima, lakini kujua kilichoendelea hadi kuzuia watu kwends kumuona na kukusanyika kwa maombi makanisani, dhambi hiyo haitamwacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…