Furaha Dominic: Rais Samia awe mwangalifu na hao waliomzunguka, wengi wao ni Wafitinishi (KUPE) walimdanganya Magufuli!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Furaha Dominic ambaye ni mpwa wa hayati Magufuli aliyegombea ubunge jimbo la Kawe na kushika nafasi ya kwanza huku Pascal Mayalla akiwa wa 162 amesema siku atakayokutana na Rais Samia atampa orodha ya Wafitini wote waliomzunguka.

Furaha anadai CCM kumejaa siasa chafu za kupakana matope, kufitinishana, kuchongeana na kusingiziana huku KUPE wa chama wakimnyonya damu Rais.

Furaha amesema ameshuhudia mengi sana katika utawala wa mjomba wake (Magufuli) ikiwemo yeye mwenyewe kudhibitiwa na kikundi cha Wasiojulikana ili asigombee ubunge

Furaha alikuwa akihojiwa na Aloyce Nyanda katika kipindi cha The Big Agenda, Star tv.

Mjadala ulikuwa mkali na Furaha alionekana akifuta machozi mara kwa mara huku mtangazaji Mtozi akimfariji.
Mahijiano yataendelea tena Ijumaa kwani jana hayakukamilika.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Kama Furaha analizwa na CCM wewe ni nani hadi Uchekelee?
 
Huyo analizwa na kifo cha mjomba wake kwani bila shaka aliahidiwa kacheo lakini sasa ameona ile ahadi imeyayuka.
 
Ni kweli kabisa anayosema huyo Furaha, watu wamekalia fitna, majungu na kupakaziana kashfa za ajabu ajabu !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…