Habari wanabodi
Mimi ndugu yenu naishi maisha ya kawaida tu, ashukuriwe muumba nina kipato cha kuweza kubadili mboga na kadhalika, naamini nimependelewa kuliko wengi wanaonizunguka, sitaki kujikweza lakini si haba (ashukuriwe aliye juu).
Naishi maisha ya kawiada (common man life), tatizo ninaloliona ninakuwa sina furaha yaani naishi tu lakini sifurahii. Nikikumbuka miaka karibia 10 iliyopita nikiwa chuo au nyuma zaidi sikuwa na kitu lakini nilikuwa na furaha sana, hustle bustle za chuo, Msosi wa mpaka jero lakini maisha yalikuwa matamu. Kwasasa kila kitu kipo, familia ninayo na vitu muhimu vinavyomzunguka binadamu kwa karne ya 21 ninavyo au ninauwezo navyo lakini sina furaha,tatizo sijui ni lipi?
Marafiki sina kwasasa wale wa enzi hizo wengi tumepotezana (sijui kama hili ni tatizo), familia ipo na haina migogoro tupo tu tunaishi katika hali ya kawaida hakuna maajabu kawaida sana. Je, tatizo ni nini?
Nifanyeje ili niweze kuwa nafuraha kama zamani? Maisha yangu ya sasa ni kazi na familia hamna cha ziada...sina michepuko naona hata nikiwa naye hautanisaidia.
Naomba ushauri tafadhali.