Furaha ni nini? Nitaipataje furaha?

Furaha ni nini? Nitaipataje furaha?

Duksi

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
229
Reaction score
576
Habari wanabodi

Mimi ndugu yenu naishi maisha ya kawaida tu, ashukuriwe muumba nina kipato cha kuweza kubadili mboga na kadhalika, naamini nimependelewa kuliko wengi wanaonizunguka, sitaki kujikweza lakini si haba (ashukuriwe aliye juu).

Naishi maisha ya kawiada (common man life), tatizo ninaloliona ninakuwa sina furaha yaani naishi tu lakini sifurahii. Nikikumbuka miaka karibia 10 iliyopita nikiwa chuo au nyuma zaidi sikuwa na kitu lakini nilikuwa na furaha sana, hustle bustle za chuo, Msosi wa mpaka jero lakini maisha yalikuwa matamu. Kwasasa kila kitu kipo, familia ninayo na vitu muhimu vinavyomzunguka binadamu kwa karne ya 21 ninavyo au ninauwezo navyo lakini sina furaha,tatizo sijui ni lipi?

Marafiki sina kwasasa wale wa enzi hizo wengi tumepotezana (sijui kama hili ni tatizo), familia ipo na haina migogoro tupo tu tunaishi katika hali ya kawaida hakuna maajabu kawaida sana. Je, tatizo ni nini?

Nifanyeje ili niweze kuwa nafuraha kama zamani? Maisha yangu ya sasa ni kazi na familia hamna cha ziada...sina michepuko naona hata nikiwa naye hautanisaidia.

Naomba ushauri tafadhali.
 
Mimi sio mwanasaikolojia. Ila kutokana na maelezo yako nimegundua vitu hivi:

1. Wakati upo chuo ulikua na furaha ingawa haukua na hela wala FAMILIA.

2. Ulipomaliza chuo ukapata kazi (kwahiyo na hela) na kisha UKAOA (familia) ila tatizo hauna furaha.

Kwa kucheki hapo juu vitu vilivobadirika ni Kupata hela na Kuoa.

Sidhani kama chanzo cha ukosefu wa furaha yako ni Kupata Hela. Me naamini iko NAMBA MBILI.

ANZIA HAPO.
 
We Unataka urudie hali ya utotoni wakati una mvi.

Ile hali ya kishkaji shule huwa haitokeagi tena ukishakuwa baba / mama.

Bali wewe ndo unapaswa uwape wanao.
 
"Inside every old man, is a young child, who wonders what happened!?" - Author Unknown
 
"If you take the life's lie out of a common man, straight-away you take his happiness." - Henrik Ibsen
 
Ulipokuwa chuo ulikuwa huna kitu lakini ulikuwa na furaha NI UWONGO MKUBWA... Ambao walikuwa hawana kitu hata chuo wameshindwa ku-Afford.
 
Mkuu kipo kinachokufanya ukose furaha ila hujataka kukisema,katika hii hela unayopata au katika familia uliyoianzisha,lakini usikwepe majukumu wala usitamani kupata zaidi ya upatacho kwa njia mbaya.kiguse kidogo kinachokufanya ukose furaha ni kipi,ndio ushaurike vzr
 
Mkuu jua kwamba furaha yako inatoka ndni ya nafsi yako.

Sio mazingira ya nje ndo yanaleta furaha no,bi ni mazingira ya ndani(nafsi)ndo yanaleta furaha.

Kwa sababu kuna watu wanadhani wakiwa na kazi pamoja na familia basi watakuwa na furaha,wakati huo wewe unavyo hivyo vyote lakini huna furaha.

Sasa laiti kwma ingekuwa kwamba mazingira ya nje ndio yanaleta furaha basi na wewe automatically ungekuwa na furaha tu kwa sababu mazingira yako ya nje kuna watu wanayataka kwa kudhani wakiwa nayo watapata furaha.

Mifano ni mingi lakini furaha ni state of mind.

Kuna 2atu walidhani kuwa ku2a k2ao chuo 2anasoma kwa kukumoaa na huku wakipata mpaka ugali wa jero basi walidhani kuwa mazingira hayo ndio sababu ya huzuni zao ama kutokuwa na furaha. Lakini wewe ulikuwa na furaha wakati upo katikw mazingira hayo hwyo ambwyo wengine yaliwakosesaha furaha.

Laiti ingelikuwa huzuni inatokana na mazingira ya nje basi watu wote ambao walipotia mazingira ya chuo kama wewe wangekuwa na huzuni,lwkini tumeona wewe hukuwa na huzuni,hivyoazingira hayakuweza kukuathiri wewe wakati huo huo wengine waliathiriwa na mazingira hayo.

Utagunfua kuwa furaha na huzuni ni jambo linabaki katika uamuzi wako mwemyewe.

Wanaume wengi wakishaoa wanajikuta hawana furaha kwa sababu kila siku wanazidi kuwazoea wake zao na kuwaona sio chochote ni kama wanawakw wengine wakati mwanzo waliwaona ni wazuri.

Hali hii inamuathiri mume mpaka katika mambo mengine anaona hakuna jambo jipya katika maisha anakuwa bored kabisa wengine wanaomba mpaaka wake zao wafe ili aow wazuri wengime,lakini ni akili tu zimewafanya kuwa hivyo.

Nina mengi ya kuandika lakini niishie hpa kwanza
 
Soma nyuzi za chizi maarifa,kidukulilo,zero brain etc, alafu uludi kunishukuru
 
Kuipata furaha ni changamoto kubwa sana kwa binaadam wa kileo, Kukosa furaja kunahusisha mlolongo mrefu sana.

Jifunze kusahau mambo yaliyopita yaache kama yalivyo huwezi kuyabadili yaache angalia mbele.

Jisamehe wewe mwenyewe wasamehe wengine waliokukosea kwa kujua au kutokujua.

Usishikilie vitu moyoni kama hasira,wivu,kibri,uchoyo,unafiq,kusengenya nk..
Toa shukrani.

Kila siku shukuru kwa ajili ya familia ,Afya,Kazi,nk..taratibu hali itabadilika..tilia mkazo katika msamaha na usahau.
 
Kuna kitu umekikosa ambacho ni uwepo MUNGU
Ndio maana unahisi huna furaha mkaribishe MUNGU kwenye maisha yako kuwa na furaha itakuwa sio optional ni lazima

Mithali 12:20 Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.
Jaribu hili
 
Mkuu jua kwamba furaha yako inatoka ndni ya nafsi yako.

Sio mazingira ya nje ndo yanaleta furaha no,bi ni mazingira ya ndani(nafsi)ndo yanaleta furaha.

Kwa sababu kuna watu wanadhani wakiwa na kazi pamoja na familia basi watakuwa na furaha,wakati huo wewe unavyo hivyo vyote lakini huna furaha.

Sasa laiti kwma ingekuwa kwamba mazingira ya nje ndio yanaleta furaha basi na wewe automatically ungekuwa na furaha tu kwa sababu mazingira yako ya nje kuna watu wanayataka kwa kudhani wakiwa nayo watapata furaha.

Mifano ni mingi lakini furaha ni state of mind.

Kuna 2atu walidhani kuwa ku2a k2ao chuo 2anasoma kwa kukumoaa na huku wakipata mpaka ugali wa jero basi walidhani kuwa mazingira hayo ndio sababu ya huzuni zao ama kutokuwa na furaha. Lakini wewe ulikuwa na furaha wakati upo katikw mazingira hayo hwyo ambwyo wengine yaliwakosesaha furaha.

Laiti ingelikuwa huzuni inatokana na mazingira ya nje basi watu wote ambao walipotia mazingira ya chuo kama wewe wangekuwa na huzuni,lwkini tumeona wewe hukuwa na huzuni,hivyoazingira hayakuweza kukuathiri wewe wakati huo huo wengine waliathiriwa na mazingira hayo.

Utagunfua kuwa furaha na huzuni ni jambo linabaki katika uamuzi wako mwemyewe.

Wanaume wengi wakishaoa wanajikuta hawana furaha kwa sababu kila siku wanazidi kuwazoea wake zao na kuwaona sio chochote ni kama wanawakw wengine wakati mwanzo waliwaona ni wazuri.

Hali hii inamuathiri mume mpaka katika mambo mengine anaona hakuna jambo jipya katika maisha anakuwa bored kabisa wengine wanaomba mpaaka wake zao wafe ili aow wazuri wengime,lakini ni akili tu zimewafanya kuwa hivyo.

Nina mengi ya kuandika lakini niishie hpa kwanza
Nashukuru kwa maelezo mazuri, nadhani wengi hatuijui hio nadharia ya furaha hutoka ndani...pengine chnagamoto ni kipi ufanye ili furaha itoke ndani?
 
Back
Top Bottom