FURSA: Biashara ya Airport Shuttle Dar (JNIA) 2 Ubungo/Tegeta/ CBD/Mbagala

FURSA: Biashara ya Airport Shuttle Dar (JNIA) 2 Ubungo/Tegeta/ CBD/Mbagala

Andrew123

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2012
Posts
8,358
Reaction score
10,976
Wajasiriamali hebu kamateni fursa ya kuanzisha Airport Shuttle mnaanzia pale Airport na ku-drop watu ama Ubungo/mwenge/Tegeta halafu nyingine ielekee Temeke/Mbagala/Kongowe na nyingine Kimara/Kibamba maana kuchukua taxi za Airport ni maumivu pia kukwea boda boda/bajaj sasa hiv zishakatazwa
 
Hili wazo sio geni,nakumbuka iliwahi kuanzishwa hii huduma sijui yule muwekezaji aliishia wapi.
i
 
wale madereva taxi airport hawataki kusikia habari ya shuttle na wengi wao ni WACHAWI a.k.a VIGAGULA ukijidai unaingiza Shuttle mule ndani airport tarajia kugeuzwa CHIZI

hahahaa, ukiwa mwoga kiasi hicho unafikiri kuna biashara utafanya?!!...kama kuchoma vitumbua wanarogana, unafikiri utafanya biashara gani? weka gari pale, tangaza biashara yako vizuri, ongeza na huduma zingine kama escort na booking za hotel na guest house kwa wageni watakuonea juujuu tu hauna muda wa kuungua jua kama wao.
 
mi huwa naendaga na NOAH yangu nasubiria abiria wa fastjet wakitoka tu natangaza 5,000 UBUNGO - MWENGE. kuna siku dereva taxi mmoja akanishtukia. Akaenda kuwaita wenzake wanileteee Fujo kisa naharibu biashara yao nikawazingua kuwa hao ni kwaya imekuja kurekodi DVD
 
Wazo zuri. Mtu anayejua jinsi ya kupata kibali cha hiyo biashara pale airport atujuze
 
hakuna haja ya kibali ingiwa pale tega mingo ukisubiria fastjet au Emirates ikitua utapata vichwa vingi sana ila uwe mjanja maana wale madreva taxi wakikushtukia unapiga Taxi Bubu hawachelewi kukurushia mawe
 
mi huwa naendaga na NOAH yangu nasubiria abiria wa fastjet wakitoka tu natangaza 5,000 UBUNGO - MWENGE. kuna siku dereva taxi mmoja akanishtukia. Akaenda kuwaita wenzake wanileteee Fujo kisa naharibu biashara yao nikawazingua kuwa hao ni kwaya imekuja kurekodi DVD

We boy.a mwongo sana.
 
achene wivu nyie watanzania. blessings ni mjasiriamali na halalamiki humu nyie mnaishia kuponda tu tuambieni mmefanya nini kuongeza kipato?
 
pale JNIA kumekaa kimazabe zabe sana hasa wale madreva taxi (wengi mno) na ni waswahili wasiopenda mabadiliko kama alivyosema mmoja wa wachangiaji unaweza kulogwa pale usikuwa makini. CHUKUA TAHADHARI
 
Back
Top Bottom