NANGA WA DEPO
JF-Expert Member
- Oct 8, 2014
- 917
- 1,201
Wakuu ,, Heri ya Mwaka mpya!!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,, ninae kijana wa kiume wa ndugu yangu ambae amemaliza darasa la saba mwaka Jana lakini kwa bahati mbaya hakufanya vizuri na hivyo hakuchaguliwa kuendelea na sekondari ,,kiukweli NIDHAMU yake ndio haswa inanisukuma nimsaidie.
Huyu dogo nimeletewa akiwa darasa saba mwishoni tayari alishakuwa na msingi mbovu , haikua rahisi kumbadilisha katika hii late stage.
Lakini ningeanza nae tangu darasa la kwanza nina uhakika asingefeli.
Nilijaribu kumsomesha pre-form one mwaka Jana , kwamba akiwa na muelekeo mzuri nimpeleke sekondari hata za private. Lakini kiukweli uwezo wake ni dhaifu sana nahisi atapoteza mda. Mimi naamini elimu ni elimu tu aidha iwe ni formal au informal atafanikiwa tu hata kama hatasoma sekondari.
Nlijaribu kwenda kuulizia kozi pale VETA lakini kwa elimu yake ni kozi ya Ufundi ujenzi, udereva na Ushonaji ndizo zinafaa ,,,, kozi zingine wanataka waliomaliza form iv.
Nimelazimika kuishi nae kwa sababu Fulani Fulani hivi kama mnavyojua
Maisha haya kusaidiana tu ....Mimi mwenyewe sikulelewa na wazazi wangu.
Kuhusu kozi au biashara kaniruhusu nimchagulie kwa sababu yeye hana uzoefu na maisha.....ila yuko tayari kufanya kwa moyo chochote nitakachomchagulia.
Naomba tushirikishane fursa ya biashara au kozi gani asomee.
Nina kianzio cha laki tatu kwa sasa.
Sent using Jamii Forums mobile app