Fursa gani inamfaa kijana aliyehitimu darasa la 7?

Fursa gani inamfaa kijana aliyehitimu darasa la 7?

NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
917
Reaction score
1,201
Wakuu ,, Heri ya Mwaka mpya!!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu,, ninae kijana wa kiume wa ndugu yangu ambae amemaliza darasa la saba mwaka Jana lakini kwa bahati mbaya hakufanya vizuri na hivyo hakuchaguliwa kuendelea na sekondari ,,kiukweli NIDHAMU yake ndio haswa inanisukuma nimsaidie.

Huyu dogo nimeletewa akiwa darasa saba mwishoni tayari alishakuwa na msingi mbovu , haikua rahisi kumbadilisha katika hii late stage.
Lakini ningeanza nae tangu darasa la kwanza nina uhakika asingefeli.

Nilijaribu kumsomesha pre-form one mwaka Jana , kwamba akiwa na muelekeo mzuri nimpeleke sekondari hata za private. Lakini kiukweli uwezo wake ni dhaifu sana nahisi atapoteza mda. Mimi naamini elimu ni elimu tu aidha iwe ni formal au informal atafanikiwa tu hata kama hatasoma sekondari.

Nlijaribu kwenda kuulizia kozi pale VETA lakini kwa elimu yake ni kozi ya Ufundi ujenzi, udereva na Ushonaji ndizo zinafaa ,,,, kozi zingine wanataka waliomaliza form iv.

Nimelazimika kuishi nae kwa sababu Fulani Fulani hivi kama mnavyojua
Maisha haya kusaidiana tu ....Mimi mwenyewe sikulelewa na wazazi wangu.

Kuhusu kozi au biashara kaniruhusu nimchagulie kwa sababu yeye hana uzoefu na maisha.....ila yuko tayari kufanya kwa moyo chochote nitakachomchagulia.

Naomba tushirikishane fursa ya biashara au kozi gani asomee.
Nina kianzio cha laki tatu kwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
-Siamini katika Formal education ili mtu afanikiwe katika biashara/ujasiriamali

-Ila pia ni ukweli usiopingika kama huyo dogo ni mvivu hata wa kujiendeleza kidogo kielimu..basi hiyo ni empty set tu, hatotoboa hata uongeze sifuri katika huo mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke VETA akasomee fani yenye uwezo wa mchezaji namba nane uwanjani.
Usimpeleke kwenye kozi za upepo kama zinavyonadiwa na magufuli atakosa cha kufanya akuibie.
.
ANGALIZO; mpeleke VETA na sio vyuo vinavyosimamiwa na VETA.
 
Ndio mkuu,,nafikiri ni malezi Fulani aliyolelewa.

Lakini kwa sasa nimelazimika kuishi nae kwa sababu Fulani hivi.

Maisha haya kusaidiana tu Mimi ,,,mwenyewe sikulelewa na wazazi wangu.

Ok.

-Kwasasa ningeshauri apate ujuzi wowote ule ambao yeye atahisi unamfaa.

-Kama msimamo wenu ni biashara, kwa mtaji huo ni kama fursa kwake kupata ujuzi tu. Ila unachoweza kufanya mfungulie biashara itayomuwezesha kushurubika ipasavyo ili apate senti mia.

-Mfano wa biashara ndogondogo ambazo hatosumbuliwa na TRA..mpe mashine ya manual ya kusaga miwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke VETA akasomee fani yenye uwezo wa mchezaji namba nane uwanjani.
Usimpeleke kwenye kozi za upepo kama zinavyonadiwa na magufuli atakosa cha kufanya akuibie.
.
ANGALIZO; mpeleke VETA na sio vyuo vinavyosimamiwa na VETA.
Naomba kamfano mkuu kuhusu hizo fani za mchezaji namba nane na kozi za upepo kama hutojali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kamfano mkuu kuhusu hizo fani za mchezaji namba nane na kozi za upepo kama hutojali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa umri wake najua hana zaifi ya miaka 15 hivyo akisomea mechanics mpaka apate diploma ambapo atakuwa NONDO sana kuliko vijana wa auto mobile pale NIT atakuwa na miaka 19-20 hata wenzie waliokwenda kidato cha kwanza watasubiri.
.
Fani zingine ambazo sip za kutegemea ajira zinacheza kiungo na zinashambulia ni ELECTRICAL (wa magari na majumbani) plumbing, na UJENZI!
 
Asante sana...

Ingawa hata Mimi nilikuwa napenda sana aende machenics tatizo ni kwamba wanatakiwa form iv kusoma kozi hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asome hiyo ya fundi cherahani, wanawake na hata baadhi ya wanaume wanashona sana, unavyońa biashara ya vitenge inashamiri vingi vinaenda kushonea nguo, hata uniform za shule bado ni dili zuri, cha msingi ahakikishe anakuwa fundi bora.
 
Enzi zetu kwa wale waliokuwa vichwa vigumu walikuwa wanapelekwa garage kujifunza ufundi kisha akishakuwa na kimo na nidhamu anafundishwa gari baada ya hapo anaachiwa mtaani na kuna jamaa nawajua wana maisha yao sasa smart kabisa ila hawakusoma.

Maisha yoyote kama anao uwezo wa kujifunza vitu vipya nadhani hutokosa pakumshikiza ili umsaidie.

Sent using Redmi Note 5
 
Asante mkuu...
Nashukuru namuona anao uwezo wa kujifunza vitu vipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asome hiyo ya fundi cherahani, wanawake na hata baadhi ya wanaume wanashona sana, unavyońa biashara ya vitenge inashamiri vingi vinaenda kushonea nguo, hata uniform za shule bado ni dili zuri, cha msingi ahakikishe anakuwa fundi bora.
Pia akiwa mbunifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kama darasani ni sifuri aangalie ana kipaji gani.Muendeleze kwenye kipaji chake,mfano muziki,mpira wa mguu,kupigana n.k
 
Back
Top Bottom