GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Nikumbushe kisa kimoja cha ukweli kabisa ingawa ni cha siku nyingi. Yupo mchaga mmoja ambaye alikuwa amebahatika kupata ajira hapa Jijini, baada ya muda fulani akaamua kutafuta sehemu ambayo alifungua banda la chipsi. Alimwita mdogo wake kutoka nyumbani Moshi akamweka hapo. Baada ya Muda fulani yule bwana akapata Likizo, akaamua kumsaidia mdogo wake shuguli za chips.
Kwa mapato aliyoyaona muda huo mfupi akashtuka sana, akaamua kuacha kazi ili afanye
biashara hiyo ya Chipsi jambo ambalo lilileta mzozo na baba yake mzazi ambaye hakukubaliana kabisa na mpango huo huku akisisitiza kuwa yeye hakumsomesha aje kuuza chipsi.
Yule mchaga hakukubali, akaacha kazi na akafungua 'senta' nyingine ya Chipsi.....
Tuachane na huyo mchaga hebu nirudi kwenu wadau naomba tupeane uzoefu hapa
ni fursa gani ambazo macho ya kawaida haizioni kuwa Fursa za maana lakini zinaweza
kukupaisha Kimaisha?