Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

Fursa gani zinadharauliwa lakini zinaweza kukutoa kimaisha?

fursa zinatofautiana kulingana na mahali ulipo, ila hii isikupite: kufuga samaki, kulima vanilla, kulima vegetables, kuwaagizia watu mizigo nje ya nchi kwa faida, kumiliki frames za kukodisha kwa wafanyabiashara, kulima vitunguu saumu na tangawizi, etc
Kulima vegetable aina gani?
 
Uuzaji wa samaki toka mkoani kwenda dar Kariakoo na masoko mengineyo, inalipa mno!
Hasa maeneo ya Manzese Madizini kuna fursa kubwa sana mtaji wako ni baiskeli
 
Industry yenye moto ss iv ni e-sports ( online video game competition) video games kwa ujumla, artificial intelligence na crypto currencies, kwa kifupi kutatua changamoto za watu kwa kutumia technolojia.Kati ya hizi nilizotaja mm nimewekeza kwenye video games, zina addiction viby kwaiyo pesa zinanifata tu zenyewe. Toka nimeanza hii wiki ya tatu nahisi, minimum kwa siku haishuki chini ya 40k.
Mkuu unaweza kutolea maelezo hapo kwenye online video games inakuaje?
 
Niaje
Jaribu ku google most expensive liquid/scorpion vernom wanatumia kutengenezea insulin na mambo kibao nikikutajia bei ya lita tano ya hiyo sumu ya n'nge hutoamini kwa kifupi wanunuzi wanakufata wenyewe sasa kuna mibongo naielezea hapo juu hainielewi imekariri biashara ni kuuza mitumba inasikitisha sana
kaka niaje naweza kupata contact zako tuwasilianr naona nimeielewa hii biashara
 
Kuna kamji flani niliwahi kupita. Kuna wamama na wadada wanafanya biashara ya uji jioni, nilipokaa na kuongea na dada mmoja aliniambia kwa siku anaweza laza mpaka 15,000/= faida.
 
Jamani kuna kuku nimeona hapa south Africa ni wakubwa sio kawaida. Paja kama la mtoto mchanga !!! Sijui kwa nini hii mbegu haijaletwa bongo?
 
Unaweza kutengeneza genge ukaliweka likawa la kisasa zaidi. Genge halidanganyi. Au kuchoma chapati jioni eneo la karibu na chuo

8f653362a1a625ed5845c425710dfbbc--caribbean-food-fruit-stands.jpg
 
Kila sIku nafikiria kuanzisha biashara ya kukaanga mihogo maeneo ya Posta. Mihogo yenyewe inaweza kuwa sio fursa sana ila fursa itakuwa kwenye matangazo ya hiyo muhogo.Nitatangaza kuwa mihogo hii inaongeza nguvu za kiume. Hapo ndipo fursa ilipo..
[emoji1] [emoji2]
 
Nikumbushe kisa kimoja cha ukweli kabisa ingawa ni cha siku nyingi. Yupo mchaga mmoja ambaye alikuwa amebahatika kupata ajira hapa Jijini, baada ya muda fulani akaamua kutafuta sehemu ambayo alifungua banda la chipsi. Alimwita mdogo wake kutoka nyumbani Moshi akamweka hapo. Baada ya Muda fulani yule bwana akapata Likizo, akaamua kumsaidia mdogo wake shuguli za chips.

Kwa mapato aliyoyaona muda huo mfupi akashtuka sana, akaamua kuacha kazi ili afanye
biashara hiyo ya Chipsi jambo ambalo lilileta mzozo na baba yake mzazi ambaye hakukubaliana kabisa na mpango huo huku akisisitiza kuwa yeye hakumsomesha aje kuuza chipsi.

Yule mchaga hakukubali, akaacha kazi na akafungua 'senta' nyingine ya Chipsi.....

Tuachane na huyo mchaga hebu nirudi kwenu wadau naomba tupeane uzoefu hapa
ni fursa gani ambazo macho ya kawaida haizioni kuwa Fursa za maana lakini zinaweza
kukupaisha Kimaisha?
Haha ha ha ha ha Watu wanawachukulia kuku Rahisi sana!! Kuku wanalipa sana lakini
sio mtaji wa kitoto ule, Inatakiwa ukaze msuli kwelikweli uache mambo yako mengi na
uwe na 'usiriasi' hautaki masihara, nikianza kuelezea hapa ninavyowajua wanJF wataanza
kuniuliza kwanini umeacha kufuga.
Biashara zote zina uzito sawa kiuwajibikaji. Biashara zote zina fursa sawa za kukupa mafanikio. Biashara zote zinahitaji kiwango sawa cha uwekezaji ili kukupa kiwango cha mafanikio unayoyataka. Biashara zote zina nafasi ya kukua kutoka hatua moja hadi nyingine. Biashara zote zinawezekana kufanikisha malengo yangu kwa kuzingatia wakati, mazingira, soko lengwa na jinsi ulivyojidhatiti kuiendesha biashara yako.
 
Back
Top Bottom