Fursa: Mifuko ya nailoni imepigwa marufuku ni Wakati wetu sasa kutafuta kitu mbadala

sidhani kama kuna paperbag ya kubeba tikiti maji au boga kwa mfano,sasa sijui babu zetu waliishije kabla ya plastic bag,as kwa kubeba kikapu haiwezimake,nani atakuwa anabeba kikapu mtaani mda wote,inabidi twende semina elekezi zanzibar kwanza
Mkuu paperbag za kubeba hivyo ulivyovitaja hapo juu zipo. Tatizo litakuja kwenye bei. Ninasema hivyo maana nimeona kwa majirani zetu Kenya hiyo mifuko ipo lakini ni ghali ambapo mteja wewe ndiye unayelazimika kuununua na sio sehemu ya huduma kutoka kwa muuzaji wa bidhaa kama tulivyozoea. Mfano Kenya ukienda buchani nyama unafungiwa kwenye karatasi lakini karatasi hiyo ni maalum hailowanishwi na maji maji au damu ya nyama.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inabidi wauzaji wawe na viroba kama vile vya kuwekea Unga vya kg 10, ikiwezekana wawe wanaviuza maana ni sh 500 tu, maana mifuko ya plastic kweli ni changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbadala ni kutengeneza reusable bags kubwa ambazo watu watauziwa na kuzitumia tena na tena na tena.
Nafikiri mtatengeneza za hivyo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Si tulikuwa na vikapu kabla ya haya mazagazaga? Kwanini visirudi? Mifuko ya vitambaa pia ambayo unaweza kutumia mara chungu nzima.

 
Hapo utaihitaji kiroba cha katani, utafanya kujitwisha tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhindi huko kwao wana vimifuko vimetengenezwa kwa material ya kamba zinaitwaga JUTE,zingine material Ya KATANI , hizi zinaoza na ni ngumu kuliko Rambo, pia size kubwa kuliko Rambo duka lolote unalokwenda zipo ila zinauzwa, wao wanachofanya wananunua kabisa hiyo bag unakaa nayo Home kwa ajili Ya shopping, ukitaka kwenda sokoni unaibeba hiyo bag yako uliyohifadhi
Conclusion:
huto tumifuko twa karatasi ni special kufungia chipsi kavu na mishkaki vibandani. Full replacement ya "Marlboro" ni kitu kingine kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbadala ni kutengeneza reusable bags kubwa ambazo watu watauziwa na kuzitumia tena na tena na tena.
Nafikiri mtatengeneza za hivyo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hii REUSABLE BAGS hata Mimi naona ndio mbadala chamsingi itolewe elimu kwa wanajamii materials zinazotumika tuongeze viwanda hii kwa wajasiliamali ni sahihi na salama sana
 
Majani makavu ya migomba tuliyokuwa tunatumia kufungia vyakula kama nyama, samaki, mboga na kila kitu virudishwe ama siyo kila mtu aende na kikapu kilichotengenezwa na majani ya mawese, nshongolwa na vitu vingine ambavyo ni organic. Tuliweza zamani why not now. Ulaya kuna bag unanunua ambayo unatumia muda wote unapokwenda suppermarket na unapewa point kwa kuitumia. Asia nchi zimeanza kutumia hata majani ya migomba na palm leaves.
 
Mtaona watu wakatavyo buni mifuko mbali mbali ya karatasi?
Material ni karatasi,gundi,kamba ya katani.....kwishneyy

Unaweza pia tumia karatasi aina ya Manila au kitambaa kwa nje kutengenezea mifuko na kwa ndani ukaweka plastic,kishikio kwa juu ukaweka kamba ya katani mfuko tayari

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…