Fursa: Mifuko ya nailoni imepigwa marufuku ni Wakati wetu sasa kutafuta kitu mbadala

Fursa: Mifuko ya nailoni imepigwa marufuku ni Wakati wetu sasa kutafuta kitu mbadala

sidhani kama kuna paperbag ya kubeba tikiti maji au boga kwa mfano,sasa sijui babu zetu waliishije kabla ya plastic bag,as kwa kubeba kikapu haiwezimake,nani atakuwa anabeba kikapu mtaani mda wote,inabidi twende semina elekezi zanzibar kwanza
Mkuu paperbag za kubeba hivyo ulivyovitaja hapo juu zipo. Tatizo litakuja kwenye bei. Ninasema hivyo maana nimeona kwa majirani zetu Kenya hiyo mifuko ipo lakini ni ghali ambapo mteja wewe ndiye unayelazimika kuununua na sio sehemu ya huduma kutoka kwa muuzaji wa bidhaa kama tulivyozoea. Mfano Kenya ukienda buchani nyama unafungiwa kwenye karatasi lakini karatasi hiyo ni maalum hailowanishwi na maji maji au damu ya nyama.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mantiki yako nilivokuelewa ni kuwa:
Either inabidi tuwe tunatembea na makapu mitaani, ili ikitokea unahemea vitu usipate tabu ya kurudi nyumban kufata kikapu.

La sivyo, tuwe tunaingia gharama kununua makapu mengi each time tuko mbali na home na tunataka tuhemee. Yaani assume unataka kununua kilo tatu za mchele (mfano tu) hakuna mfuko wa karatasi unahimili mzigo huo. Hivo basi itakubidi hapohapo dukani ununue kikapu (cha 5,000 kwa mfano) ili ubebee mzigo wako.

Does it make sense???
Inabidi wauzaji wawe na viroba kama vile vya kuwekea Unga vya kg 10, ikiwezekana wawe wanaviuza maana ni sh 500 tu, maana mifuko ya plastic kweli ni changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbadala ni kutengeneza reusable bags kubwa ambazo watu watauziwa na kuzitumia tena na tena na tena.
Nafikiri mtatengeneza za hivyo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Si tulikuwa na vikapu kabla ya haya mazagazaga? Kwanini visirudi? Mifuko ya vitambaa pia ambayo unaweza kutumia mara chungu nzima.

Habari za hapa wakuu

Kama mnavyojua mifuko ya plastic(nylon) zote zimepigwa marufuku miezi michache baadae zitaacha kutumika,hilo haliondoi sababu kwamba lazima watu madukan wapimiwe sukari,unga,maharagwe,mandazi n.k nusu,robo,kilo n.k

Vijana hii ni fursa kwetu kuja na idea nzuri yakureplace mifuko ya nylon,inatumika sana,soko ni uhakika kwa 95%.

Kwa upande wa kufungia vitu dukan nina idea ya zile bahasha flani hivi nyepesi za kakii...kwa wale wanaonda kuchukua vitafunwa kwenye migahawa mikubwa na ya kati wanazijua. Bahasha flani hivi kama za pembe nne, ile ni fursa ndugu zangu.

Nawakaribisha wataalamu wa mambo wanaojua upatikanaji wa mashine ya kutengeneza zile bahasha,bei, n.k

Karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
fikirini nje ya box nyie, acheni ushamba!!!
kwahiyo mnategemea hizo karatasi zenu ndio ziwe full replacement ya mifuko ya "Rambo/Marlboro".

assume umeenda kwa soko umenunua mchele kilo 3, unga kilo 2 na nusu, ndizi robo mkungu, nyanya za 1500, na chainizi za 1000 (ambazo hazijakatwa katwa). Je, hutu tukaratasi twenu tunaweza kuhimili vitu hivyo???

mmeona sasa ambavo hamfikirii nje ya box.
Hapo utaihitaji kiroba cha katani, utafanya kujitwisha tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muhindi huko kwao wana vimifuko vimetengenezwa kwa material ya kamba zinaitwaga JUTE,zingine material Ya KATANI , hizi zinaoza na ni ngumu kuliko Rambo, pia size kubwa kuliko Rambo duka lolote unalokwenda zipo ila zinauzwa, wao wanachofanya wananunua kabisa hiyo bag unakaa nayo Home kwa ajili Ya shopping, ukitaka kwenda sokoni unaibeba hiyo bag yako uliyohifadhi
Conclusion:
huto tumifuko twa karatasi ni special kufungia chipsi kavu na mishkaki vibandani. Full replacement ya "Marlboro" ni kitu kingine kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbadala ni kutengeneza reusable bags kubwa ambazo watu watauziwa na kuzitumia tena na tena na tena.
Nafikiri mtatengeneza za hivyo

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
Hii REUSABLE BAGS hata Mimi naona ndio mbadala chamsingi itolewe elimu kwa wanajamii materials zinazotumika tuongeze viwanda hii kwa wajasiliamali ni sahihi na salama sana
 
Majani makavu ya migomba tuliyokuwa tunatumia kufungia vyakula kama nyama, samaki, mboga na kila kitu virudishwe ama siyo kila mtu aende na kikapu kilichotengenezwa na majani ya mawese, nshongolwa na vitu vingine ambavyo ni organic. Tuliweza zamani why not now. Ulaya kuna bag unanunua ambayo unatumia muda wote unapokwenda suppermarket na unapewa point kwa kuitumia. Asia nchi zimeanza kutumia hata majani ya migomba na palm leaves.
 
Mtaona watu wakatavyo buni mifuko mbali mbali ya karatasi?
Material ni karatasi,gundi,kamba ya katani.....kwishneyy

Unaweza pia tumia karatasi aina ya Manila au kitambaa kwa nje kutengenezea mifuko na kwa ndani ukaweka plastic,kishikio kwa juu ukaweka kamba ya katani mfuko tayari

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom