Fursa Mpya kwa Tanzania! Starlink Kuleta Mapinduzi ya Intaneti kwa Bei Nafuu na Ubora wa Juu

Fursa Mpya kwa Tanzania! Starlink Kuleta Mapinduzi ya Intaneti kwa Bei Nafuu na Ubora wa Juu

Nimeuliza Kwa mapinduzi gani hayo waliofanya Kundustan? Tanzania inaongoza Kwa Watumiaji wa internet
Mkuu Tanzania inaongoza kwa sababu ya wingi wa watu lakini sio kwa ubora wa internet ama matumizi ya internet. Tanzania ina watumiaji wengi wa internet kuliko hata Netherland ama Finland kwa sababu ya wingi wa watu lakini huwezi kusema Tanzania imeendelea kwenye matumizi ya digitali kuliko Netherland.

Kwenye masuala ya digitalization na matumizi ya internet kubadilisha maisha ya watu Kenya wako mbali sana kuliko Tanzania.
 
Kaka starlink itarahisisha sana huduma vijijini kupata mtandao wa uhakika, tofauti na sasa ambapo kuna vijiji kupakua file la hata 10mb ni mtihani. Mjini itatukomboa tunaohitaji internet yenye kasi na bei rafiki.
Sio vijijini tu, hapa Dar mjini ni changamoto kubwa sana.

Kwa speed ya internet ya Starlink, hakuna hata fixed cable internet company ambayo itashindana na Starlink.

Hawa jamaa wakipata upinzani watachangamka.

Kama laki 1 napata GB1034 kwa mwezi kwa speed kubwa hivyo na data ikiisha kabla ya mwezi kuisha nauziwa GB 1 kwa shilingi 400, huku Vodacom wananiuxia GB 1 kwa shilingi elfu 2100, nitake nini tena.
 
Kasi sawa, ila bei rafiki? Watafunga branch za Bank, makampuni makubwa makubwa ya kimataifa etc. Ila Mtanzania wa kawaida hawezi ku afford starlink
 
Waombaji ni wengi mnapagawa na starlink
Mkuu waombaji ni wengi kweli ila Starlink inakua na faida zaidi kuliko wengine kwa sababu ya speed yake, urahisi wake na tayari Starlink imeshajijengea hesahima ya kua mtandao wenye kasi zaidi wa satelite Duniani.
 
Sio vijijini tu, hapa Dar mjini ni changamoto kubwa sana.

Kwa speed ya internet ya Starlink, hakuna hata fixed cable internet company ambayo itashindana na Starlink.

Hawa jamaa wakipata upinzani watachangamka.

Kama laki 1 napata GB1034 kwa mwezi kwa speed kubwa hivyo na data ikiisha kabla ya mwezi kuisha nauziwa GB 1 kwa shilingi 400, huku Vodacom wananiuxia GB 1 kwa shilingi elfu 2100, nitake nini tena.
Hio 2100 huuziwi GB1 mzee unauziwa 650MB ambazo zimekuwa masked kama 1GB. These guys think we are silly.

Ndio maana utashangaa ukitumia mtandao flani 1GB hiyo hiyo inamaliza week ila mitandao mingine hata siku haiishi umejiunga kifurushi cha week mara 3
 
Ni kweli kwamba gharama ya ufungaji wa Starlink inaweza kuonekana kuwa ya juu mwanzoni, lakini ni muhimu kuelewa kwamba bei hizi zinaweza kushuka kadiri teknolojia inavyoendelea na ushindani unavyozidi kuongezeka. Katika nchi kama Kenya, Starlink imeanza kutoa huduma kwa bei ambayo, ingawa bado ni juu kuliko watoa huduma wa siku zote kina voda na ndugu zake, inatoa faida kubwa zaidi kutokana na kasi ya intaneti na upatikanaji wake hata katika maeneo ya mbali. Hii inawalenga zaidi wale ambao wana changamoto za kupata huduma za intaneti za kawaida.

Katika Tanzania, tunapaswa kutarajia kwamba ushindani kati ya Starlink na watoa huduma wa ndani utasaidia kupunguza bei kwa muda. Pia, Starlink inatoa huduma ya intaneti ya kasi ambayo itawafaidi Watanzania wengi, si tu "mafisadi". Teknolojia hii inalenga kufikia watu wa kawaida, hasa wale walioko vijijini au maeneo ambayo miundombinu ya intaneti bado haijaboreshwa.

Kwa hiyo, ingawa gharama ya awali inaweza kuonekana kuwa kubwa, faida zitakuwa wazi: intaneti ya kasi, upatikanaji wa huduma katika maeneo magumu kufikiwa, na hatimaye, gharama zinazoweza kushuka kadiri huduma inavyozidi kusambaa nchini. Watanzania wengi wataweza kufurahia huduma hii, hasa katika zama hizi ambapo intaneti imekuwa hitaji la msingi kwa elimu, biashara, na mawasiliano.

Starlink ni nzuri kuwa nayo Tanzania, itasaidia sana kusambaza internet services ya uhakika kwa haraka sana, but on other side tukumbuke kuna mkongo wa Taifa, ambayo serikali imeweka billions of investment, so ni bora tukawa nazo zote alafu watumiaji yaani wananchi wataamua kuchagua ipi, na Starlink sio bei rahisi sana kama watu wanavyodhania, ni bei sawa tu na mitandao ya simu hapa Tz, labda faida kubwa ya Starlink ni uhakika wa Speed, yaani kama ni 100Mbs ni kweli 100Mbs au 150Mbs iko stable hivyo ukilinganisha na mitandao yetu ya Tz..!!

Overall ni hatua nzuri sana, tuipokee kwa mikono miwili..!!
 
Sio vijijini tu, hapa Dar mjini ni changamoto kubwa sana.

Kwa speed ya internet ya Starlink, hakuna hata fixed cable internet company ambayo itashindana na Starlink.

Hawa jamaa wakipata upinzani watachangamka.

Kama laki 1 napata GB1034 kwa mwezi kwa speed kubwa hivyo na data ikiisha kabla ya mwezi kuisha nauziwa GB 1 kwa shilingi 400, huku Vodacom wananiuxia GB 1 kwa shilingi elfu 2100, nitake nini tena.
Kwa kasi tunayoambiwa hata ukiuziwa laki na hamsini sawa tu, sio kono kono za mjini hapa.
 
Starlink ni nzuri kuwa nayo Tanzania, itasaidia sana kusambaza internet services ya uhakika kwa haraka sana, but on other side tukumbuke kuna mkongo wa Taifa, ambayo serikali imeweka billions of investment, so ni bora tukawa nazo zote alafu watumiaji yaani wananchi wataamua kuchagua ipi, na Starlink sio bei rahisi sana kama watu wanavyodhania, ni bei sawa tu na mitandao ya simu hapa Tz, labda faida kubwa ya Starlink ni uhakika wa Speed, yaani kama ni 100Mbs ni kweli 100Mbs au 150Mbs iko stable hivyo ukilinganisha na mitandao yetu ya Tz..!!

Overall ni hatua nzuri sana, tuipokee kwa mikono miwili..!!
Mkuu kukishakua na uhakika wa ubora, bei sio tatizo. Bei ni sawa ila ubora tofauti, hapo ndio utofauti ulipo. Sio hilo tu, upatikanaji wake ni wa uhakika uwe popote, kichakani, mlimani, porini huko Selous, uwe barabarani unatembea ni wewe tu mzigo unashuka kama kawaida.
 
Hio 2100 huuziwi GB1 mzee unauziwa 650MB ambazo zimekuwa masked kama 1GB. These guys think we are silly.

Ndio maana utashangaa ukitumia mtandao flani 1GB hiyo hiyo inamaliza week ila mitandao mingine hata siku haiishi umejiunga kifurushi cha week mara 3
Mkuu tunaibiwa mchana kweupe jua limewaka. Na hawa jamaa hawataki ije Starlink. Kumbuka hata Rais wa Kenya juzi hapa akiwa New York Marekani alitoa siri kwamba Safaricom ya Kenya na wenzake walipinga ujio wa Starlink kwamba utawaingilia kwenye soko na kuwaharibia soko. Baadae serikali ilipowagomea wakashusha bei ya vifurushi na kuongeza kasi ya internet yao.

We should expect the same hapa Bongo mzee. Vodacom hela waliyoniibia kwa miaka 17 sasa itaelekea mwisho. Nanunua ki min starlink changu natembea nacho popote basi.
 
Wakuu wa Jamii Forums,
Nina habari njema sana kwa nchi yetu! Tanzania ipo mbioni kupokea huduma za intaneti kupitia satelaiti kutoka kampuni ya Starlink. Hatua hii ni fursa muhimu kwa Watanzania wote, na ni nafasi yetu kutoa maoni yetu chanya kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuunga mkono mchakato huu. Unaweza kutuma maoni yako kwa barua pepe kupitia dg@tcra.go.tz.
View attachment 3152698
Kuingia kwa Starlink nchini kunaleta ushindani wa moja kwa moja kwa watoa huduma wetu wa ndani kama Vodacom, Tigo, na Airtel, na hii inamaanisha huduma za intaneti zitakuwa bora zaidi na bei zitaweza kupungua kwa Watanzania wote. Fikiria jinsi gani intaneti itakuwa nafuu zaidi na yenye kasi, siyo tu mijini, bali pia vijijini, na hata maeneo ya mbali kama Hifadhi ya Serengeti na Tarangire. Sasa, hatutokuwa na changamoto ya mawasiliano katika maeneo haya!

Fursa za Ajira na Maendeleo

Kufikika kwa intaneti ya Starlink nchini Tanzania kutafungua milango kwa ajira nyingi za mtandaoni na shughuli mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo:

Uundaji wa maudhui ya kidigitali: Wasanii na wabunifu sasa wanaweza kuendeleza vipaji vyao na kufikia hadhira kubwa zaidi kwa urahisi.

Kamari za mtandaoni, Forex, na sarafu za kidigitali: Kwa wenye ujuzi na maarifa ya kufanya biashara mtandaoni, fursa zitakuwa nyingi na rahisi kwa sababu ya intaneti imara na ya haraka.

Programu za masomo mtandaoni: Wanafunzi na watafiti kutoka sehemu yoyote nchini wataweza kupata elimu ya kidigitali kwa urahisi.

Kazi za mbali: Starlink itawawezesha Watanzania kushiriki katika ajira za kimataifa, kutoa huduma za kitaalam mtandaoni, na kujiendeleza kiuchumi.

Faida kwa Serikali na Sekta Mbalimbali

Starlink haitaleta tu huduma bora kwa wananchi, lakini pia itasaidia serikali kwa kuongeza mapato kupitia kodi zitokanazo na shughuli za mtandaoni. Kwa kuwa na intaneti bora, hospitali zetu zitaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, na sekta ya utalii itafurahia maendeleo makubwa kwa kuwa wageni wataweza kufurahia mawasiliano hata wanapokuwa ndani ya hifadhi zetu.

Ni Muhimu Kwa Nini Kutoa Maoni Chanya kwa TCRA?

Kwa miaka mingi, baadhi ya watoa huduma wa ndani hawajatujali watumiaji wa kawaida na wamekuwa na gharama kubwa za huduma, huku ubora wa intaneti ukiwa chini. Ni wazi kuwa huduma bora kwa bei nafuu kwa wote imekuwa ndoto kwa muda mrefu. Kuingia kwa Starlink kutaleta ushindani mzuri na kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora kwa gharama nafuu.

Sasa ni wakati wetu kuchukua hatua! Tuma maoni yako chanya kwa TCRA kupitia barua pepe kwa dg@tcra.go.tz na tuwaunge mkono Starlink kuleta mapinduzi ya mawasiliano nchini Tanzania.

Pamoja tunaweza kujenga taifa lenye intaneti bora kwa wote!
Kwahiyo tutahitajika kununua line ya starlink ili tuweze kuaccess hii internet au

Mnielekeze
 
Gharama ni mwanzo tu, mbona Zuku ilianza kidogo kidogo ila imeenea kila kona ya kariakoo. Imagine watu walio subscribe Zuku wanalipisha buku unaunganishwa siku nzima unlimited. Hio ni kariakoo
 
Back
Top Bottom