Fursa Mpya kwa Tanzania! Starlink Kuleta Mapinduzi ya Intaneti kwa Bei Nafuu na Ubora wa Juu

Nimeuliza Kwa mapinduzi gani hayo waliofanya Kundustan? Tanzania inaongoza Kwa Watumiaji wa internet
Mkuu Tanzania inaongoza kwa sababu ya wingi wa watu lakini sio kwa ubora wa internet ama matumizi ya internet. Tanzania ina watumiaji wengi wa internet kuliko hata Netherland ama Finland kwa sababu ya wingi wa watu lakini huwezi kusema Tanzania imeendelea kwenye matumizi ya digitali kuliko Netherland.

Kwenye masuala ya digitalization na matumizi ya internet kubadilisha maisha ya watu Kenya wako mbali sana kuliko Tanzania.
 
Kaka starlink itarahisisha sana huduma vijijini kupata mtandao wa uhakika, tofauti na sasa ambapo kuna vijiji kupakua file la hata 10mb ni mtihani. Mjini itatukomboa tunaohitaji internet yenye kasi na bei rafiki.
Sio vijijini tu, hapa Dar mjini ni changamoto kubwa sana.

Kwa speed ya internet ya Starlink, hakuna hata fixed cable internet company ambayo itashindana na Starlink.

Hawa jamaa wakipata upinzani watachangamka.

Kama laki 1 napata GB1034 kwa mwezi kwa speed kubwa hivyo na data ikiisha kabla ya mwezi kuisha nauziwa GB 1 kwa shilingi 400, huku Vodacom wananiuxia GB 1 kwa shilingi elfu 2100, nitake nini tena.
 
Kaka starlink itarahisisha sana huduma vijijini kupata mtandao wa uhakika, tofauti na sasa ambapo kuna vijiji kupakua file la hata 10mb ni mtihani. Mjini itatukomboa tunaohitaji internet yenye kasi na bei rafiki.
Kasi sawa, ila bei rafiki? Watafunga branch za Bank, makampuni makubwa makubwa ya kimataifa etc. Ila Mtanzania wa kawaida hawezi ku afford starlink
 
Waombaji ni wengi mnapagawa na starlink
Mkuu waombaji ni wengi kweli ila Starlink inakua na faida zaidi kuliko wengine kwa sababu ya speed yake, urahisi wake na tayari Starlink imeshajijengea hesahima ya kua mtandao wenye kasi zaidi wa satelite Duniani.
 
Hio 2100 huuziwi GB1 mzee unauziwa 650MB ambazo zimekuwa masked kama 1GB. These guys think we are silly.

Ndio maana utashangaa ukitumia mtandao flani 1GB hiyo hiyo inamaliza week ila mitandao mingine hata siku haiishi umejiunga kifurushi cha week mara 3
 

Starlink ni nzuri kuwa nayo Tanzania, itasaidia sana kusambaza internet services ya uhakika kwa haraka sana, but on other side tukumbuke kuna mkongo wa Taifa, ambayo serikali imeweka billions of investment, so ni bora tukawa nazo zote alafu watumiaji yaani wananchi wataamua kuchagua ipi, na Starlink sio bei rahisi sana kama watu wanavyodhania, ni bei sawa tu na mitandao ya simu hapa Tz, labda faida kubwa ya Starlink ni uhakika wa Speed, yaani kama ni 100Mbs ni kweli 100Mbs au 150Mbs iko stable hivyo ukilinganisha na mitandao yetu ya Tz..!!

Overall ni hatua nzuri sana, tuipokee kwa mikono miwili..!!
 
Kwa kasi tunayoambiwa hata ukiuziwa laki na hamsini sawa tu, sio kono kono za mjini hapa.
 
Mkuu kukishakua na uhakika wa ubora, bei sio tatizo. Bei ni sawa ila ubora tofauti, hapo ndio utofauti ulipo. Sio hilo tu, upatikanaji wake ni wa uhakika uwe popote, kichakani, mlimani, porini huko Selous, uwe barabarani unatembea ni wewe tu mzigo unashuka kama kawaida.
 
Mkuu tunaibiwa mchana kweupe jua limewaka. Na hawa jamaa hawataki ije Starlink. Kumbuka hata Rais wa Kenya juzi hapa akiwa New York Marekani alitoa siri kwamba Safaricom ya Kenya na wenzake walipinga ujio wa Starlink kwamba utawaingilia kwenye soko na kuwaharibia soko. Baadae serikali ilipowagomea wakashusha bei ya vifurushi na kuongeza kasi ya internet yao.

We should expect the same hapa Bongo mzee. Vodacom hela waliyoniibia kwa miaka 17 sasa itaelekea mwisho. Nanunua ki min starlink changu natembea nacho popote basi.
 
Kwahiyo tutahitajika kununua line ya starlink ili tuweze kuaccess hii internet au

Mnielekeze
 
Gharama ni mwanzo tu, mbona Zuku ilianza kidogo kidogo ila imeenea kila kona ya kariakoo. Imagine watu walio subscribe Zuku wanalipisha buku unaunganishwa siku nzima unlimited. Hio ni kariakoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…